October 29, 2020

 


KIKOSI cha Azam FC kesho kina kazi ya kusaka pointi tatu muhimu mbele ya JKT Tanzania kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex.


Azam FC inashuka uwanjani ikiwa na kumbukumbu ya kupokea kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar,  mchezo uliochezwa Uwanja wa Jamhuri, Morogoro. 


Inakutana na JKT Tanzania iliyotoka kushinda mabao 6-1 mbele ya Mwadui FC, Uwanja wa Mwadui Complex. 


Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa maandalizi yapo vizuri ila watawakosa nyota wawili Kwenye mchezo huo 


"Obrey Chirwa na Oscar Masai wataukosa mchezo wa kesho wa Azam FC dhidi JKT Tanzania, wote ni majeruhi ila maandalizi na kila kitu kipo sawa," amesema.


Chirwa ndani ya Azam FC amefunga mabao manne na pasi mbili za mabao, Masai ametoa pasi moja ya bao.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic