UONGOZI wa Simba umesema kuwa unazidi kujiweka sawa kwa ajili ya kutetea taji lao la Ligi Kuu Bara walilotwaa msimu wa 2019/20 kwa sababu wana kikosi imara na chenye wachezaji wazuri wenye ushirikiano.
Tayari imecheza mechi tano kwa msimu wa 2020/21, imekusanya pointi 13 baada ya kushinda mechi nne na kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na Mtibwa Sugar, Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.
Meneja wa Simba, Patrick Rweyemamu amesema kuwa mpango mkubwa wa timu hiyo ni kuweza kutwaa tena ubingwa kwa msimu wa 2020/21.
"Tuna mechi nyingi na ngumu hasa ukizingatia kwamba ligi ina ushindani mkubwa hilo lipo wazi ila malengo yetu ni kuona kwamba tunashinda mechi zetu na kupata matokeo mazuri.
"Sababu kubwa ya sisi kufanya hivyo ni kuwa na kikosi kizuri ambacho kinapata matokeo kwa kadri ambavyo kinahitaji, mbinu na ushirikiano ndani ya Simba ni vitu vinavyotupa mafanikio," amesema.
Ikiwa imecheza jumla ya mechi tano na kufunga mabao 14 kinara wao wa utupiaji ni Meddie Kagere mwenye mabao manne.
Na Jambo kubwa na la muhimu vilevile litalothibitisha ubingwa ni utulivu na nidhamu ya hali ya juu na mahaba ya moyoni ya kwelikweli ya wana Simba bila ya chokochoko au hiyana kwa timu yao
ReplyDeleteMahaba ya Gazeti hili kwa Simba yamepitiliza mjiangalie kuna hatari mkapunguza wasomaji wa GAZETI lenu
ReplyDeleteHapana sio kweli ndugu yangu kwamba gazeti hili lina mahaba yalopitiliza kwa Simba. Tutofautishe Blog na Gazeti. Hii ni Blog ya Saleh Jembe ambayo kwa asilimia zaidi ya 80% inajitahidi kuweka mizani sawa katika taarifa za vilabu na ligi zetu za Tanzania. Lakini gazeti la Championi ndilo naona lina tatizo la mahaba hususani kwa club ya Yanga ambapo hata wakati Yanga inapokuwa haina jambo la maana utakuta habari kubwa ktk gazeti la Championi ni Yanga tu. fuatilia tu utaona na utakubaliana na mimi.
DeleteKaeni hivohivo na porojo Leno na wengine wakikata mbuga
ReplyDeleteSimba Ni vitendo tu, ooo! Mwandishi hao timuatimua makocha wanasemaje!? Waandike
ReplyDelete