HUKU Mkurugenzi wa Uwekezaji wa GSM na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga, Injinia Hersi Said, akisema kuwa watamtangaza rasmi Mrundi, Cedric Kaze kuwa ndiye Kocha Mkuu wa timu hiyo, hivi karibuni kocha huyo aliwapigia simu mastaa wa timu hiyo, wakiwa kambini akiwemo Carlos Carlinhos.
Matajiri hao tayari wamefanikisha kulipitisha jina hilo huku akiyapoteza majina mawili ikiwa ni George Lwandamina wa Zambia na Mjerumani, Ernest Middendorp aliyekuwa anaifundisha Kaizer Chiefs.
Yanga wamefikia hatua ya kumleta Kaze ambaye rekodi zake zinaonyesha kuwa amefundisha ndni ya ya Akademi ya Barcelona baada ya kufikia makubaliano ya kuachana na aliyekuwa Kocha Mkuu wa timu hiyo, Mserbia, Zlatko Krmpotic.
Hata hivyo, baada tu ya kupitishwa chanzo cha ndani kinasema kuwa aliomba namba za wachezaji wote wa timu hiyo na tayari ameshaanza kazi ya kuwapa majukumu mmoja baada ya mwingine.
“Sijui nani alimpa namba, lakini alianza kuwapigia simu mchezaji mmoja baada ya mwingine na kuwaeleza nini cha kufanya.
“Hapo inaonekana ndiyo kashaanza kazi hivyo kwa inavyoelezwa ni kwamba anawafahamu Simba na alikuwa akifuatilia kila kitu kwa muda mrefu, ameongea na kila mchezaji na kumueleza mapungufu yake na nini cha kufanya,” kilisema chanzo hicho cha ndani.
Baadhi ya mastaa wa Yanga ambao inadaiwa amewapigia simu ni pamoja na Lamine Moro, Mukoko Tonombe, Carlos Carlinhos, Bakari Mwamnyeto na Tuisila Kisinda.
Hata hivyo, Hersi ambaye hakulizungumzia hilo la kocha huyo kupiga simu, yeye alilieleza Championi kuwa, huyu ndiye anapewa asilimia kubwa ya kuwa kocha wa timu hiyo ya Jangwani.
“Uongozi wa Yanga utafanya kikao cha mwisho kabla ya kumtangaza Cedric Kaze, kama kocha mkuu.
“Kaze na Yanga tupo katika hatua za mwisho za yeye kusaini na kuja kuifundisha timu yetu baada ya kuachana na Zlatko tuliyefikia makubaliano mazuri.
“Kabla ya mchezo wetu wa watani wa jadi, Simba kocha wetu Kaze atakuwa nchini kuishuhudia timu yake ikiwa uwanjani,” alisema Hersi.
Kocha huyu mwenye historia kali ya soka la Afrika amewahi pia kuifundisha Akademi ya Barcelona ya Hispania na anapewa nafasi ya kufanya mambo makubwa anatua nchini wikiendi hii.
Awali alikubaliana na Yanga mwanzoni mwa msimu lakini akashindwa kutua nchini kutokana na matatizo ya kifamilia
We salehe kuwa professional basi unatulisha matango pori vipi bwana upenzi usikuondoe kwenye reli .
ReplyDeleteAmefundisha akademi ya Barcelona huku sasa mi jobless yupo Canada.Kakosa hata timu ya daraja la 3?Tutalishwa tango wanayanga mpaka tukome.Hatuna cha kusema kuhusu GSM. Wametukalia haswa.
ReplyDelete😆😆😆😆
Deletewalianza kwa aliyetimuliwa kuwa ni kocha wa makombe tena wameamia na huyu tena si kocha wa makombe bali ni kocha aliyefundisha barcelona mm jicho kodo
ReplyDelete