October 11, 2020

 



TIMU ya Taifa Tanzania ya Tanzania leo imepoteza kwa kufungwa bao 1-0 kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Burundi uliochezwa Uwanja wa Mkapa.


Kwenye mchezo wa leo ambao mgeni rasmi alikuwa ni Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kipindi cha kwanza timu zote mbili zilitoshana nguvu baada ya kwenda vyumba vya kubadilishia nguo wakiwa hawajafungana.


Kipindi cha pili mambo yalizidi kuwa magumu kwa timu zote mbili ambapo Stars ilijaribu kufanya mashambulizi yalishindwa kuzaa matunda na Burundi ilikuwa ya kwanza kupiga shuti la kwanza ambalo lililenga lango kipindi cha pili.


Bao pekee la ushindi lilipatikana dakika ya 84 kupitia kwa Said Ntibazonkiza na kuwafanya Burundi kuibuka na ushindi ugenini.

Simon Msuva nyota wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars amesema kuwa haikuwa bahati kwao kwa kuwa walipambana ili kupata ushindi ila mambo yalikuwa magumu kwao.


Stars ilimaliza dakika 90 ikiwa pungufu baada ya kiungo mkabaji Jonas Mkude kuonyeshwa kadi nyekundu dakika ya 78 kwa kuwa alikuwa alionyeshwa kadi mbili za njano.



11 COMMENTS:

  1. Kocha kapanga kikosi cha ovyo kbixa
    hafai wachezaji km mzamiru na ulimwengu unawafanyia sabu mda umekwisha ndo nn?
    ni ujinga , uzezeta na upumbafu kbisa

    ReplyDelete
    Replies
    1. Haswaa hiyo kero yangu,sure boy hakupaswa kucheza japo mkude nidham mbovu,alijua anakadi ya njano akafanya ufala.

      Delete
  2. Nilisema mapema kabla ya mechi hakuna timu hapo

    ReplyDelete
  3. Kocha wa stars ni boya

    ReplyDelete
  4. Shida yetu ni usimba na uyanga mpaka kwenye national teams! Tunawapanga wachezaji kinazi na sio kimichezo

    ReplyDelete
  5. Sio shida usimba na uYanga kocha tayari keshaingizwa kwenye siasa za kwamba kila mchezaji wa timu fulani lazima apangwe taifa stars.Hata mimi nilijiuliza inakuwaje kocha anamuacha nje Muzamiru Yasini muda wote ule na mechi ya kirafiki tu? Kwangu mimi bila ya kuficha Iddi Nado kwenye mechi ya ushindani siwezi kumuacha Muzamiru Yasini nje nikampanga Nado.sio kwamba Nado sio mchezaji mzuri ila yupo weak au hayopo vizuri kinguvu ni mchezaji anaeopaswa kuingia kipindi cha pili wakati wa wachezaji wa upande wa pili wameshapungua kasi.Namuona kocha mbishi wa simba Sven asietaka ujinga wa kuingiliwa kwenye majukumu yake ndie anatufaa kwa taifa stars. Lakini ikiwa Burundi tumecheza vile Tunisia itakuwaje? Watatufirigisa kweli kweli.

    ReplyDelete
  6. Taifa inahitaji mechi nyengine ya kujipima nguvu kabla ya Tunisia

    ReplyDelete
  7. Kwa bahati mbaya mpira ni mchezo wa wazi, tumeshazoea kucheza mpira wa magazetini

    ReplyDelete
  8. Kabisa kwanza hakuna kitu mechi ya kirafiki katika mpira uwanjani. Ikiwezekana wachezaji wanatakiwa kukaza zaidi kwenye mechi ya maandilizi kuliko kwenye mechi ya ushindani na ndivyo walivyofundishwa warundi na kuja kutuaibisha nyumbani na ndio maana wachezaji au timu zetu mara kadhaa zimekuwa zikimchefua JPM. sababu hawapo siriasi.Bila ya kuwa siriasi na kitu unachokitaka sahau kabisa kukipata.Mentality au uangalifu wa mchezaji ukiwa wa kilegealegea kwenye mechi ya kirafiki usidhani itakuja kubadilika kwenye mechi ya mashindano mtoto uleavyo ndivyo akuavyo.

    ReplyDelete
  9. Ingawa team yetu ilicheza vzr bahati haikuwa yetu nilichokoiona Jana hapakuwa na strike ya Kati Kati mipira mingi waliiwahi jamaa na kuiondoa pia raise man hawakuwa sawa kabisa kwa baadhi ya offside ingawa pia kocha alijaa na hasira mapema hawezi kucontrol mchezo na pia team yetu kipindi Cha pili hawakuwa mchezoni kabisa ndio maana tukafungwa pia tuliloose na kukosa kujiamini alipotoka mkude lkn lawama kubwa kwa mkude aliigharimu team lkn hata kocha nitamlaumu kwa uchache viungo aliwapanga wa kudifence sana huwezi kuweka ndemla na mkude Kati halafu unataka Faisal apande mbele team itaelemewa Sana kocha hawajui vzr wachezaji aliokua anawatoa na anaowaingixa maana zile sub za kuchelewa vile Bora hasingefanya sub kabisa maana waliongia hawakutekeleza majukumu ingawa wengine waliingia too late

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic