FT: Mpira umekamilika Uwanja wa Uhuru kwa Yanga kusepa na pointi tatu mazima mbele ya Polisi Tanzania.
Yanga 1-0 Polisi Tanzania
Uwanja wa Uhuru
Dakika ya 90 Tunombe anapewa huduma ya kwanza
Dakika ya 89 Manyika anaokoa hatari na Sarpong anakosa bao
Dakika ya 85 Yanga wapo mbele kwa bao moja
Dakika ya 77 Farid Mussa anatoka anaingia Zawad Mauya
Dakika ya 75 Nchimbi anapeleka mashambulizi Polisi Tanzania
Dakika ya 70 Tonombe Mukoko anafunga Goool la kwanza na kuwanyanyua ananchi
Dakika ya 66 Farid Mussa anafanya jaribio linaokolewa
Dakika ya 61 Pato Ngonyani anaonyeshwa kadi ya njano
Dakika ya 58 Kaheza anaanzisha mashambulizi kwenda Yanga
Dakika ya 57 Ditram Nchimbi anaingia anatoka Haruna Niyonzima
Dakika ya 55 Manyika anaanzisha mashambulizi kwenda Yanga
Dakika ya 53, Haruna Niyonzima anapeleka mashambulizi Polisi Tanzania
Dakika ya 48 Moro anaokoa
Dakika ya 47 Kisinda anachezewa faulo inapigwa na Kibwana Shomari
Kipindi cha pili kimeanza Uwanja wa Uhuru.
Farid Mussa anafanya jaribio la mapema halizai matunda
Uwanja wa Uhuru:- Yanga 0-0 Polisi TanzaniaKipindi cha kwanza
Oktoba 22
Ligi Kuu Bara
Dakika 45 za kipindi cha kwanza zimekamilika Uwanja wa Uhuru.
Mapumziko:-Yanga 0-0 Polisi Tanzania
Dakika ya 40 Uwanja wa Uhuru, Moro anachezewa faulo na mpira unapigwa kuelekea kwa Polisi Tz
Dakika ya 36 Lamine Moro anaokoa hatari iliyopigwa na Marcel Kaheza
Kipindi cha kwanza kinaendelea kwa sasa baada ya dakika moja ya kupoza koo kukamilika.
Dakika moja kwa ajili ya kupoza koo na joto la Dar, Uwanja wa Uhuru.
Kona ya kwanza ilipigwa na Tuisila Kisinda kona ya pili Farid Mussa zote hazizai matunda.
Dakika ya 15: Bado ngoma ni ngumu kwa timu zote mbili Uwanja wa Uhuru.
Dakika ya 14:-Farid Mussa anampa Fei Toto
Yanga wanapiga kona ya pili
Kisinda anacheza faulo
YANGA ipo Uwanja wa Uhuru ikisaka pointi tatu mbele ya Polisi Tanzania
Msimamo wa ligi ukoje?
ReplyDeleteYanga anaoongoza anakaribia kuchukua ubingwa zikiwa zimebaki mechi mbili tu ligi kuisha
ReplyDeleteUkiona kimyaaa ujue simba kafa
ReplyDeleteNA UKIONA KELELE NYINGI UJUE WANATAKA KWENDA FIFA NA CAS
Delete