CEDRIC Kaze, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa amekipanga kikosi chake kupata ushindi mbele ya Tanzania Prisons kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa Uwanja wa Uhuru.
Leo Oktoba 22, Yanga itaikaribisha Polisi Tanzania kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa Uwanja wa Uhuru majira ya saa 10:00 jioni.
Kaze ambaye amesaini dili la miaka miwili Yanga akichukua mikoba ya Zlatko Krmpotic ana kibarua kizito cha kuvunja rekodi ya Yanga kushindwa kusepa na pointi tatu kwenye mechi zao mbili msimu wa 2019/20.
Mechi ya kwanza iliyochezwa Uwanja wa Uhuru zilitoshana nguvu kwa kufungana mabao 3-3 na ile ya pili walifungana bao 1-1 Uwanja wa Ushirika Moshi.
Akizungumza na Saleh Jembe, Kaze amesema kuwa anatambua namna Polisi Tanzania ilivyo hasa kutokana na mwendo wake ndani ya ligi kuwa mzuri kwa muda wote alioifuatilia.
“Wengi wanaitazama mechi yetu dhidi ya Simba lakini kuna timu inaitwa Polisi Tanzania hii nayo ni ngumu na nzuri hasa kutokana na mwendo wake ulivyo nina amini kwamba kazi itakuwa kubwa kusaka pointi tatu ila tupo tayari.
“Mashabiki wajitokeze kwa wingi, hakuna haja ya kuhofia wapinzani wetu, tutapambana na kusaka pointi tatu muhimu sapoti yao ndani ya uwanja ni muhimu pia,” alisema Kaze.
0 COMMENTS:
Post a Comment