October 3, 2020


LIGI Kuu Tanzania Bara kwa sasa ipo mzunguko wa tano ambapo rekodi zinaonyesha kuwe kwa mizunguko minne mfululizo hakuna raundi iliyokusanya jumla ya mabao 15.

Mechi tisa kila raundi zinapigwa kusaka pointi tatu ushindani umeonekana kuzidi kuongezeka kila baada ya raundi kuisha jambo ambalo linazidi kunogesha ligi.

Mpaka sasa kwenye mizunguko minne jumla yamefungwa mabao 53 kwenye mizunguko minne ambayo imekwisha kamilika.


Mzunguko wa kwanza yalipachikwa mabao 13, mzunguko wa pili mabao 13 na mzunguko wa nne ndo ulikusanya mabao mengi ambayo ni 14 huku ule wa nne ambao umemeguka mwezi Septemba ulikusanya mabao 13.


 Kinara wa kucheza na nyavu kwa mwezi Septemba ni Prince Dube mwenye mabao matatu na pasi moja ndani ya Azam FC huku kinara wa pasi za mwisho ni Luis Miqussone wa Simba mwenye pasi nne.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic