November 19, 2020

 


AZAM FC wameibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya KMKM ya Zanzibar kwenye mchezo wa kirafiki uliochezwa jana Novemba 18 Uwanja wa Chamazi. 


Mabao ya Azam FC inayonolewa na Aristica Cioaba yalifungwa na Ayoub Lyanga dakika ya 78 akimalizia pasi ya Hamahama na bao la pili lilifungwa na Akono Akono dakika ya 90.


Langoni alikaa Benedict Haule akilindwa na Bŕunce Kangwa, Daniel Amoah na Yakub Mohamed huku kitambaaa cha unahodha kikiwa mikononi mwa mkongwe Agrey Moris.


Mchezo huo ni maalumu kwa ajili ya maandalizi ya mechi zao za ligi ambapo kwa sasa Azam FC ni vinara baada ya kucheza mechi 10 wakiwa na pointi 25 kibindoni.


Watakutana na KMC Uwanja wa Uhuru Novemba 21 saa 10:00 jioni.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic