November 2, 2020


 VINARA wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Azam FC wameanza kuipigia hesabu Dodoma Jiji kuelekea kwenye mchezo wao wa ligi utakaochezwa Novemba 5, Uwanja wa Azam Complex.


Azam FC ikiwa imecheza jumla ya mechi 9 imejikusanyia pointi 22 inakutana na Dodoma Jiji ambayo imecheza mechi 9 na kujikusanyia pointi 12 ikiwa nafasi ya 10.


Mchezo wao uliopita Azam FC ililazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya JKT Tanzania ikiwa nyumbani, Uwanja wa Azam Complex.


Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa kila kitu kipo sawa na wanaamini watapata pointi tatu mbele ya wapinzani wao.


"Siku zote uwanja wa nyumbani ni sehemu ambayo wachezaji wetu hucheza kwa kujiamini na kufurahi hasa kwa kuwa wanapata sapoti kubwa kutoka kwa mashabiki.

"Kikubwa ni kuendelea kupambana na kuona namna gani jambo letu litatimia kwa msimu huu wa 2020/21, mashabiki waendelee kutupa sapoti," amesema.


Timu ambazo zilipita Uwanja wa Azam Complex na kupoteza ilikuwa ni pamoja na Mwadui FC, Coastal Union, Polisi Tanzania.

2 COMMENTS:

  1. Azam wajitahidi la sivyo Wananchi [Yanga] wanarudi juu hapo maana wana hasira ya Nyati aliyejeluliwa...

    ReplyDelete
  2. Azam wajitahidi la sivyo Wananchi [Yanga] wanarudi juu hapo maana wana hasira ya Nyati aliyejeluliwa...

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic