November 2, 2020


 MANCHESTER United imeshuhudia maumivu tena ikiwa Uwanja wa Old Trafford kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Arsenal kwenye mchezo wa Ligi Kuu England na kufanya ikusanye jumla ya mabao 10.


Bao pekee la ushindi kwa Arsenal inayonolewa na Mikel Arteta lilipachikwa kimiani na nahodha wao raia wa Gabon, Pierre Emerick Aubameyang dakika ya 69 kwa mkwaju wa penalti uliosababishwa na kiungo Paul Pogba na kuwafanya Manchester United wasiamini wanachokiona.


Chini ya Kocha Mkuu, Ole Gunnar Solkajaer mambo yamekuwa magumu kwenye mechi za Ligi Kuu England ndani ya Uwanja wa Old Trafford kwa kuwa amepoteza jumla ya mechi tatu na kufungwa jumla ya mabao 10 huku safu yake ya ushambuliaji ikifunga mabao mawili.


United ilikubali kichapo cha mabao 3-1 dhidi ya Crystal Palace, ikachapwa mabao 6-1 dhidi ya Spurs na kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Arsenal kinakamilisha idadi ya mabao 10 wakiwa nyumbani kwa msimu wa 2020/21.  


Pogba amesema kuwa hakuwa na chaguo la kufanya zaidi kwa kuwa alikuwa akijitahidi kulinda jambo ambalo haliwezi na mwisho wa siku akafanya makosa.


"Nimefanya kosa la kijinga kabisa na sikuwa na namna kwa kuwa nilikuwa najitahidi kufanya ulinzi jambo ambalo sijalizoea ila mwisho wa siku tumepoteza nami nimefanya kosa la kijinga," amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic