TIMU ya Yanga inashuka uwanjani leo Novemba 3, 2020 kuivaa Gwambina katika mchezo wa kusaka kujiamini zaidi kwa mchezo ujao dhidi ya watani zao, Simba.
Ushindi wa Yanga leo katika Uwanja wa Gwambia utaifanya timu hiyo kukaa kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Bara licha ya sare pia inaweza kuwapa uongozi hadi matokeo ya Azam FC dhidi ya Dodoma Jiji.
Yanga imetoka kushinda bao 1-0 dhidi ya Biashara United Uwanja wa Karume.
Inakutana leo na Gwambina ambayo imetoka kupoteza kwa kufungwa mabao 3-0 dhidi ya KMC Uwanja wa Gwambina Complex.
Ni mara ya kwanza kwa timu hizi kukutana uwanjani kwenye ligi kwa kuwa Gwambina imepanda msimu huu wa 2020/21 ikitokea Ligi Daraja la Kwanza.
0 COMMENTS:
Post a Comment