NOVEMBA 7, Uwanja wa Mkapa mchezo wa dabi ya Kariakoo kati ya Yanga na Simba unatarajiwa kupigwa kuanzia saa 11:00 jioni.
Viingilio kwenye mchezo huo unaosubiriwa kwa shauku na wadau ili waweze kuona balaa la Michael Sarpong wa Yanga na Clatous Chama wa Simba ni kama ifuatavyo:- mzunguko wa rangi ya kijani ni 7,000( buku saba).
Viti vya rangi ya machungwa ni 10,000 (buku 10), VIP C ni 15,000, VIP B 20,000 na VIP A, 30,000.
Mechi za mwisho kwa timu hizi mbili zinatarajiwa kuchezwa wiki hii ambapo Yanga itamaliza kete yake ya mwisho dhidi ya Gwambina FC Uwanja wa Kirumba, Mwanza na Simba itamaliza biashara yake na Kagera Sugar, Dar.
0 COMMENTS:
Post a Comment