JACOB Masawe, nahodha wa Klabu ya Gwambina FC amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya ushindani ndani ya Ligi Kuu Bara wana imani watafanya vizuri licha ya kila timu kupambana kusaka ushindi.
Masawe ambaye ni mchezaji bora ndani ya Ligi Daraja la Kwanza kwa msimu wa 2019/20 wakati wakipambana kupanda Ligi Kuu Bara amekuwa kwenye ubora wake ndani ya ligi kutokana na uzoefu wake ambapo aliwahi kucheza pia ndani ya Stand United iliyokuwa ikishiriki ligi na alikuwa nahodha kabla ya timu hiyo kushuka daraja.
Akizungumza na Saleh Jembe, Masawe amesema kuwa kila timu inapambana kupata matokeo ndani ya uwanja jambo ambalo hata wao wanalifanya pia.
"Timu nyingi zinapambana kupata matokeo ndani ya uwanja hata sisi tunafanya hivyo, kwa sasa tunaendelea kujiweka sawa kwa ajili ya mechi zetu zijazo na tunaamini kwamba tutafanya vizuri," amesema.
Mchezo ujao kwa Gwambina inayotumia Uwanja wa Gwambina Complex kwa mechi zao za nyumbani ni dhidi ya JKT Tanzania Uwanja wa Jamhuri, Dodoma saa 8:00 mchana.
Gwambina ipo nafasi ya 14 na pointi 10 inakutana na JKT Tanzania iliyo nafasi ya 13 na pointi 10 zote zikiwa zimecheza mechi 10 ndani ya msimu wa 2020/21.
0 COMMENTS:
Post a Comment