November 19, 2020

 


LICHA ya mabosi wa Simba kuweka wazi kwamba kiungo bora ndani ya Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2019/20 Clatous Chama ni mali yao mpaka msimu wa 2022, Yanga wameweka wazi kwamba muda utazungumza.


Chama ambaye msimu uliopita alisepa na tuzo tatu, ikiwa ni pamoja na ile ya kiungo bora, mchezaji bora pamoja na kuwa ndani ya kikosi bora cha msimu wa 2019/20 anatajwa kuingia kwenye rada za Yanga kwa kile kinachoelezwa kuwa mkataba wake unameguka msimu ujao.

Kiungo huyo ambaye msimu uliopita alihusika kwenye mabao 12 kati ya 78 yaliyofungwa na Simba baada ya kutoa pasi 10 na kufunga mabao mawili, msimu huu amefunga mabao mawili na kutoa pasi tano za mabao anatajwa kuwa kwenye hesabu za Yanga.


Uongozi wa Yanga kupitia kwa Injinia Hersi Said ambaye ni Mkurugenzi wa Uwekezaji ndani ya Kampuni ya GSM ambao ni wadhamini wa Klabu ya Yanga aliweka wazi kwamba wanatambua uwezo wa Chama na wanaheshimu mkataba wake.


Ofisa Uhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz amesema kuwa kuhusu ishu ya nyota Chama licha ya Simba kuweka wazi kwamba ni mali yao muda utazungumza.


"Muda utaongea kwa kuwa wao wameweka wazi kwamba ana mkataba kwa sasa hatuwezi kusema jambo lolote lakini muda utaongea," alisema Nugaz.

7 COMMENTS:

  1. Hivi hamna cha kuandika? Kama hamna acheni kuliko kuwandanganya hao kandambili

    ReplyDelete
    Replies
    1. heeh heeh heeh.....zingekuwa habari za Mukoko kwenda simba hapo nadhani ungeshabikia sana.....ila kwakuwa ni habari za chama kwenda yanga mwandishi anaonekana ameongea utumbo.

      Delete
    2. Mbona kiwango alichoanzia chama kilikuwa chini ukilinganisha na alichoanzia Mukoko. Ligi hii tu, mbona anaonekana sio.. hata nusu ya kumsajili mukoko hafikii... hizi sifael hewa mbona zitawaua mikia kupinda!

      Delete
  2. Hivi msipoandika habari ya Chama au Mukoko mnapungukiwa mini?Tumewachoka na hizi habari za udaku.

    ReplyDelete
  3. Yaani Yanga watakuwa walizungumza na kumsainisha mchezaji mwenye mkataba??
    Hivi sheria za kuzungumza na mchezaji mwenye mkataba ni zipi?

    ReplyDelete
  4. Viongozi wa yanga hawawahurumii wapenzi wao? Kila siku wanawapiga fix hawaoni aibu?

    ReplyDelete
  5. Mwandishi hakikisha hupotoshi taarifa kuhusu tuzo alizozoa ClatoysChota Chama Jr msinuvwa 2019/2020: 1. Mchezaji bora wa Simba akapata tuzo ya Sportspesa 2 Mchezaji bora wa mashabiki wa Simba akapata tuzo hiyo 3. Mchezaji bora wa AFSC yaani madhindano ya shirikisho 4. Kiungo bora wa msimu 2019/2020 5 Mchezaji bora wa msimu 2019/2020 6. Mchezaji ndani ya kikosi cha msimu 2019/2020. Hii ndiyo dhana ya Triple C kuitwa MVP

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic