UONGOZI wa Klabu ya KMC umesema kuwa kwa sasa utaendelea kushusha dozi kwa kila timu itakayokutana nayo kwa kuwa imepata mbinu za ushindi ndani ya uwanja.
Mchezo wake uliopita ilishinda jumla ya mabao 3-0 dhidi ya Gwambina FC mchezo wao unaofuata ni dhidi ya Biashara United ya Mara.
Ofisa Habari wa KMC, Christina Mwagala amesema kuwa ushindi ambao wameupata ni salamu kwa wapinzani wao Biashara United.
"Tupo imara na kila kitu kinakwenda sawa, ushindi wetu dhidi ya Gwambina FC ni salamu tosha kwa wapinzani wetu Biashara United wajipange kupokea dozi nao pia tayari gari limewaka," amesema.
Biashara United mchezo wao uliopita waliyeyusha pointi tatu mbele ya Yanga kwa kufungwa bao 1-0.
Mchezo wao utakuwa Novemba 3 Uwanja wa Karume, Mara.
0 COMMENTS:
Post a Comment