KOCHA Mkuu wa Yanga, Cedrick Kaze amesema kuwa aliwatambua wapinzani wake ni wazito jambo lililomfanya atumie wachezaji wenye spidi mwanzo mwisho.
Mchezo huo ulikamilika kwa Azam FC kufungwa bao 1-0 na kuyeyusha jumla ya pointi tatu mazima ikiwa kwenye ngome yake ya Azam Complex.
Deus Kaseke alifunga bao la ushindi dakika ya 48 lililodumu mpaka dakika ya 90 na kumshinda mlinda mlango David Kissu.
Yanga iliibuka na ushindi huo kipindi cha pili Uwanja wa Azam Complex na kuifanya ikwee jumlajumla nafasi ya kwanza baada ya kufikisha pointi 28.
Linakuwa ni bao la kwanza kwa Kaseke ambaye ni mzawa aliyeipandisha timu yake nafasi ya kwanza kwa kuishusha Azam FC inayonolewa na Aristica Cioaba.
Kaze amesema:"Ilikuwa ni mchezo ambao unahitaji ushindani mkubwa na wachezaji wenye spidi kubwa ili kuwachosha wachezaji wa timu pinzani kwa sababu wao wengi ni wazito.
"Sasa nilipaswa kuwa nambinu ambayo ingenipa matokeo nikaanza na Kaseke ambaye alifunga bao na kutupatia pointi tatu, katika hilo ninawapongeza wachezaji wote kiujumla pamoja na mashabiki," .
Yanga inakuwa imecheza jumla ya mechi 12 ambazo ni dakika 1,080 bila kufungwa huku Azam FC ikipoteza jumla ya michezo mitatu baada ya kucheza mechi 12 ipo nafasi ya pili.
Ikiwa nafasi ya tatu, Simba na pointi zake 23 baada ya kucheza mechi 11 imepoteza mechi mbili ilikuwa mbele ya Tanzania Prisons kwa kufungwa bao 1-0 na ule dhidi ya Ruvu Shooting kwa kufungwa bao 1-0.
Ni goli siyo la kiufundi sana. Ila kupaki kwa gari la Yanga kutawagharimu kwa siku nyingine.
ReplyDeleteGoli lilikuwa la kiufundi katika vigezo vyote, kuanzia kwenye back pass ya Ditram hadi kwenye mikimbio na kross ya Yacuba na hatimaye umaliziaji wa Kaseke; kwa direct pressing.
DeleteLabda kama una matatizo mengine na hao Yanga, kitakwimu za mchezo hawakuonekana kupark basi ila style yao ya jana ililenga kuwakimbiza mabeki wa Azam, ambao ni wazito. Na hili liliwasaidia sana Yanga, Azam wakishindwa kujinasua kwenye mtego. Sub zote za Azam zilenga kuimarisha kiungo ili waushike mchezo wenzao wakawazuia mabeki wa Azam (Wadada na Kangwa) kupandisha mashambulizi.