KESHO Novemba 15 kikosi cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu, Cedric Kaze kitakuwa na mchezo wa kirafiki dhidi ya African Lyon utakaochezwa Uwanja wa Azam Complex.
Kiingilio kwenye mchezo huo wa kesho kitakachompa fursa shabiki kuona uwezo wa nyota wao Tuisila Kisinda mwenye spidi ndani ya uwanja, Paul Godfery, Abdulaziz Makame, Michael Sarpong ni buku tatu tu,(3,000).
Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh amesema kuwa maandalizi yapo sawa na wachezaji wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo unaotarajiwa kuwa na ushindani.
"Kila kitu kipo sawa ni wakati tu umebaki kushuhudia burudani kwa mashabiki hivyo wajitokeze kwa wingi kuona burudani ndani ya uwanja," amesema.
Yanga inashiriki Ligi Kuu Bara inakutana na African Lyon ambayo inashiriki Ligi Daraja la Kwanza ikiwa chini ya Kocha Mkuu, Nizar Khalfan.
0 COMMENTS:
Post a Comment