UONGOZI wa Simba umeweka bayana kuwa utafanya usajili wa kushtua kwenye dirisha dogo ambalo linatarajiwa kufunguliwa Desemba 15.
Simba chini ya Kocha Mkuu Sven Vandenbroeck ina kibarua cha kupeperusha bendera ya Taifa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo mchezo wa awali itakuwa ugenini mbele ya Plateau United ya Nigeria.
Habari zinaeleza kuwa mpango mkubwa wa Simba ni kufanya mabresho kwenye sehemu kuu mbili ikiwa ni ile ya ulinzi pamoja na kiungo.
Majina ya pacha mbili zinazokipiga ndani ya Yanga, Tuisila Kisinda na Tonombe Mukoko ambao walisaini dili la miaka miwili ndani ya Yanga wakitokea Klabu ya AS Vita yanatajwa kuwa kwenye orodha ya nyota waliopo kwenye rada.
Pia jina la kiungo mkabaji, James Kotei ambaye alikuwa ndani ya Simba na alicheza kwa mafanikio anatajwa kurejeshwa ndani ya kikosi hicho.
Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa ikitokea wakahitaji kufanya usajili basi hakuna kitachoshindikana kwa mchezaji watakayemtaka.
"Simba tukiamua jambo letu hatushindwi ila kwa sasa tunasubiri wakati wa usajili ufike tutafanya mambo makubwa na wengi watashtuka, watatikisika kwa namna ya vile ambavyo tutafanya," amesema.
Kuhusu nyota hao wa Yanga kutajwa kuibukia Simba, Injinia Hersi Said, Mkurugenzi wa Kampuni ya GSM ambao ni wadhamini wa klabu hiyo ameweka bayana kwamba nyota hao wana mikataba.
"Kuhusu Mukoko,(Tonombe) mashabiki wasiwe na mashaka ana mkataba wa miaka miwili ambao anautumikia kwa sasa hivyo wasiwe na presha," amesema.
Ninyi waandishi kuweni na weledi kwenye habari zenu mnazotuandikia. Habari za Kisinda na Mukoko kusajiliwa na Simba na Chama kusajiliwa na Yanga tumezichoka kwani hazina uhalisia hata wa 10% na ninyi kila kukicha mnatuandikia. Kwa ufupi tumewachokeni na habari zenu uchwara. Kama hamna habari za kueleweka ni bora msituandikie utumbo huu.
ReplyDeleteHuyu mwandishi kiukweli anaboa sana.
ReplyDeleteNadhan hajitambui
ReplyDeleteKwa nini kila siku usajili lazima uzue taharuki? Wachezaji wako wengi tuu, kwa nini kila mara kuanzisha ugomvi na wenzetu? Inaharabu ladha ya mpira wetu. Tafuteni wachezaji nje ya yanga na simba. Hata wachezaji wenyewe wakisajiliwa wanashindwa kucheza kwa uhuru, wanakuwa na hofu matokeo yake viwango vyao vinashuka
ReplyDeleteWachezaji wengi wautopolo hawana viwango na hadhi ya kumchezea Simba mabingwa wa nchi, kotei akirejea nisawa maana anaijua Simba na wanasimba tunamjua uwezo wake, hao wengine hawana hadhi kwa Simba yenye malengo makubwa ya sasa na baadae.
ReplyDeleteNawe pia hujitambui kabisa. Mungu Akusamehe tu maana hujitambui na unaingilia mada ambayo si ya kwako. Kwani wachezaji wenu wametokea wapi na wamelelewa mazingira gani ya kisoka mpaka wakawa na kiwango kikubwa cha kuwatisha wengine? Hawa waliobora ndio unaozungumzia na wakafungwa na Prisons na Ruvu?
DeleteUkweli unaongea Ni wachezaji wangapi wa utopolo walienda Simba wanazingua kikosi Cha kwanza moja kwa moja? ongea kimpira na Sio kinaziri. Simba mchezaji yoyote akienda utopolo anaingis first eleven direct bila maswali. Unaokota wachezaji walioexpire umfananishe na mabingwa wa nchi. Kufungwa team yoyote unaweza fungwa, mbona wewe hujafungwa lkn upo nafac ya pili na aliyefungwa yupo nafac ya kwanza. Mpira Ni mahesabu droo zitakufelisha muda si mrefu utachacha tunahesabu masaa tu. Tatu za juu unaongoza sare na magoli kiduchu alafu unasema unahadhi namabingwa wanchi ambao tayari msimu kashatwaa kombe la kwanza anaendelea kusaka mengine, wewe hata moja huna. Subiri watu wamwache mchezaji uende ukamsajili huna uwezo wa kuvunja mkataba wa mchezaji mwingine Tok as team nyingine ukamtwaa. Tutakuacha kwenye mataa muda cmrefu. Simba oyeeee! utopolo tutawabeba Tena msijali mtashiriki kimataifa mwakani * zitashiriki team nne tz michuano ya caf*
DeleteHoja zako hazina mashiko unaposema hakuna mchezaji wa Yanga awezaye kupata namba huko Mkia. Kuna beki wenu anaweza kumuweka bench Mwamnyeto au Lamin? Usiongee kwa sababu mnawakilisha nchi kimataifa ndio kuona kuwa hakuna wachezaji wa timu zingine hawana uwezo wa kuchezea kwenye timu yenu. Hata hkifuatilia vilabu vikubwa duniani vinavyochukua makombe kama ya UEFA, nk lakin kuna wachezaji wao wa kikosi cha Kwanza wakienda kwenye vilabu vingine hawawez hata kupata namba. Nadhan unavamia tu fani ya mpira; hujawah hata kucheza mpira wa makaratasi na umeanza kushabikia mpira ukubwani na huna uzoefu wa mpira hata kidogo. Usiwe una coment vitu usivyovijua kwa sababu ya ushabiki utawashushia hadhi Mikia wenzako waliokaa kimya kwa kuujua ukweli kuwa timu yenu ni ya kawaida sana na huko Ligi ya Mabingwa msipokuwa makini mtatoka mapema na kuliletea taifa aibu kama ile ya khamsa khamsa!
ReplyDeleteKama hiyo hesabu unayoisema basi sisi ndio tunaijua maana yake kwa sababu hata ukifunga goli 100 kwa mechi bado point ni zile zile 3. Sisi tumefunga machache na tumefungwa machache zaidi. Ninyi mmefunga mengi sana na hamuongozi ligi. Pia raundi ya kwanza tumecheza mechi nyingi away ninyi bado.
ReplyDelete👆 Kama hamjui faida ya magoli mengi 🤫🤫. Azam Mara ngapi msimu wamewaburuza chini kutokana na goal difference. Naona hamjui mpira maana hata umuhimu wawashambuliaji hamuujui.
ReplyDeleteHow many goals did you score? At Which position are you now? Kama unafunga magoli mengi mechi kadhaa na zingine hufungi na unaruhusu kufungwa unadhani utakuwa sawa na yule anayeshinda kila mechi japo kwa ushindi mwembamba na haruhusu kufungwa hovyo?
Delete