HITIMANA Thiery, Kocha Mkuu wa Namungo FC amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya kuiwakilisha nchi kimataifa kwenye mashindano ya kimataifa.
Namungo inaiwakilisha nchi katika Kombe la Shirikisho Afrika na mchezo wake wa awali ni dhidi ya Al Rabita ya Sudan Kusini unaotarajiwa kuchezwa kati ya Novemba 27-29 Uwanja wa Azam Complex.
Akizungumza na Saleh Jembe,Thiery amesema kuwa wanatambua kwamba ushindani ni mkubwa na kila timu inahitaji ushindi ila watapambana kufanya vizuri.
"Mashindano ya kimataifa yana ushindani mkubwa na kila timu inahitaji ushindi hilo lipo wazi nasi pia tunahitaji kupata matokeo.
"Kwa kuwa tutaanzia nyumbani tuna mtihani mkubwa wa kusaka ushindi mwanzo kwanza kisha huko tunapaswa tukalinde ushindi wetu, katika hilo tutajiweka sawa ili kupata matokeo mazuri," amesema.
0 COMMENTS:
Post a Comment