November 2, 2020


 MSHAMBULIAJI wa KMC, Relliants Lusajo, ameweka wazi kuwa mikakati yake msimu huu ni kuifungia timu hiyo mabao yasiyopungua 15 katika Ligi Kuu Bara, huku akiamini yataisaidia timu hiyo kufanya vizuri.

 

Lusajo amejiunga na KMC msimu huu akitokea Namungo ambapo msimu uliopita alimaliza ligi akifunga mabao 13, huku msimu huu akiwa na KMC amefunga mabao matatu katika michezo mitano aliyoichezea timu hiyo.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Lusajo alisema: “Malengo yangu ni kufunga mabao mengi iwezekanavyo, sitaki kuweka malengo niwe mfungaji bora ila nahitaji nifunge mabao mengi yasiyopungua 15 ambayo naamini yataisaidia timu yangu katika kujiweka kwenye nafasi nzuri.

 

“Msimu huu utakuwa na ushindani wa mabao kwa watu wengi kwa kuwa kuna ongezeko la washambuliaji wengi bora ambao licha ya kuwa bado hawajafunga, lakini naamini huko mbele watafunga sana na kuleta ushindani."

 

Lusajo mbali na kuwa tegemeo kwenye Ligi Kuu Bara, pia anatazamiwa kuiongoza safu ya ushambuliaji ya KMC kwenye mchezo ujao dhidi ya Biashara United, Uwanja wa Karume. 


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic