November 22, 2020



HAKUNA muda wa kupoteza kwa sasa ndani ya Ligi Kuu Bara kwa kuwa tayari mzunguko wa 11 umeanza kupasua anga kwa kasi baada ya jana mechi kuendelea kwenye viwanja vitatu tofauti.

 


Kazi kubwa kwa kila timu ipo kwenye kusaka ushindi ambapo kuna timu ambazo zimeanza kuonyesha dalili za kufikia mafanikio huku nyingine zikiwa zimepoteza kabisa matumaini ya kufanya vizuri.

  

Kwenye maisha ya soka suala la kukata tamaa ni kosa moja kubwa kuliko makosa mengine kwani yatafanya matokeo kuwa mabovu mpaka mwisho wa msimu.


Kupata ama kukosa ndani ya uwanja ni matokeo ambayo hayaepukiki kwa namna yoyote ile ila kikubwa ni maandalizi. Kila timu ambayo itakuwa na maandalizi mazuri inatoa fursa ya kupata matokeo chanya kwenye mechi zijazo.

 

Kabla sijafika mbali ngoja nirejee kutoa pongezi kwa mashabiki pamoja na wachezaji ambao walijitokeza kwa wingi Uwanja wa Mkapa kushuhudia mchezo wa kimataifa wa timu ya Taifa ya Tanzania dhidi ya Tunisia wikiendi iliyopita.

 

Kiukweli tumeona kwamba wachezaji walitambua umuhimu wa kupambana kusaka matokeo licha ya kushindwa kupata ushindi wa moja kwa moja na kuishia kupata sare ya kufungana bao 1-1 hilo sio jambo baya ila wanapaswa pongezi.


Makosa ambayo yameonekana benchi la ufundi ni lazima lifanyie kazi na kuweka kando sababu ambazo hazina maana katika hilo mashabiki hata hawaelewi ukija na sababu mia wao wanahitaji ushindi hakuna jambo lingine.

 

Wachezaji ambao wataitwa kwenye mechi mbili ambazo zimebaki wana kazi ya kusaka ushindi kwa hali na mali. Ili kuweza kupenya hatua ya makundi ni lazima ushindi upatikane kwani hakuna kingine kwa sasa ambacho mashabiki wanakisubiri.

 

 Ninaamini kwamba makosa yatafanyiwa kazi na mashabiki wataendelea kutoa sapoti kwa Stars kwa kuwa ni timu yetu sote. Ushindi wake ni furaha kwetu na unatufanya tuwe na furaha kila wakati na zile tofauti zetu tunaziweka kando.


Tuendelee sasa kwenye Ligi Kuu Bara pamoja na Ligi Daraja la Kwanza ambayo nayo pia inaendelea ni lazima makosa yaliyopita yafanyiwe kazi ili kuwa imara zaidi kwa wakati ujao.

 Makosa mengi walikuwa wanapewa waamuzi kwamba wanachezesha mechi chini ya viwango katika hili mamlaka husika ni muhimu kufanyia kazi haya na kuleta majibu katika makosa yaliyopita.

 

Wale ambao walikosea pia wanajukumu la kujifunza ili kuweza kuzimudu changamoto mpya. Mbali na waamuzi pia wachezaji nao wamekuwa na tabia za kupenda kugombana ndani ya uwanja.


 Ndugu zangu, mpira sio vita haina maana kwamba kwa kuwa kila timu inapambana kusaka pointi tatu ndani ya uwanja hapo mnaruhusiwa kupigana hapana.

 

Mpira ni upendo, mpira ni sehemu ya burudani, mpira ni kazi jambo ambalo linafanya watu waweze kupata mkate wao wa kila siku na kuendesha maisha yao bila matatizo yoyote yale.

 

Sasa inapotokea wachezaji wanakuwa kwenye ugomvi ambao hauna maana na kupigana ndani ya uwanja inakuwa haileti picha nzuri kwa wachezaji pamoja na mashabiki.

 Wapo wachezaji ambao wamepewa adhabu kutokana na ugomvi na wengine wamekosa mechi kadhaa ndani ya uwanja. Kukosekana kwao uwanjani ni tatizo kwa kuwa wana umuhimu wa kuwa ndani ya uwanja kutimiza majukumu yao.


Katika raundi ya 11 kwa sasa tunatarajia kuona kwamba hakutakuwa na makosa mengi ambayo yamefanyika kwenye mechi zilizopita hivyo umakini unahitajika zaidi na zaidi kwa kila mechi.

 

Haina maana kwamba hakuna makosa bali kinachotakiwa kwa waamuzi ndani ya Ligi Kuu Bara, Ligi Daraja la Kwanza ni lazima kuwe na usawa na sheria 17 zifuatwe mpira ni amani na upendo.

 

1 COMMENTS:

  1. Kabla ya kuzungumzia round ya 11 tunataka mrejesho wa adhabu walizopewa waamuzi waliochezesha mechi ya Simba na yanga maana mmekalia kimya sababu waliathirika ni Simba ingekuwa yanga kila siku mngekuwa mnarudia

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic