UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa hesabu kubwa kwa msimu wa 2020/21 ni kuona inatimiza malengo ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara na ikishindikana hapo basi watwae ubingwa wa Kombe la Shirikisho ili waiwakilishe nchi kwenye michuano ya kimataifa.
Kwa sasa Azam FC ni vinara wa Ligi Kuu Bara wakiwa na pointi 25 baada ya kucheza mechi 10,kibindoni wamekusanya jumla ya mabao 18.
Akizungumza na Saleh Jembe, Abdulkarim Amin, Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Azam FC amesema kuwa hesabu ya kwanza ilikuwa kucheza mechi zote bila kupoteza hiyo imetibuliwa ila watapambana kutimiza malengo ambayo wamejiwekea.
“Wakati tunaanza msimu tulipanga kucheza mechi zetu zote bila kufungwa hilo lilikwama baada ya kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar ila bado ninaona kwamba yapo malengo mengine ambayo tutapambana kuyafikia ikiwa ni pamoja na kutwaa ubingwa.
“Tunashiriki kwenye mashindano makubwa mawili ambayo ni Kombe la Shirikisho na Ligi Kuu Bara hapo itapendeza tukitwaa moja ama yote mawili kwa kuwa kila kitu kinawezekana na kikosi tulicho nacho ni imara,” amesema Amin.
Azam FC baada ya kucheza mechi 10 ndani ya Ligi Kuu Bara, safu ya ushambuliaji imefunga jumla ya mabao 18 na safu ya ulinzi imeruhusu mabao manne.
0 COMMENTS:
Post a Comment