November 5, 2020

 


KIUNGO mkabaji wa Simba, raia wa Brazil Gerson Fraga maarufu kama mkata umeme kwa sasa atakuwa nje kwa msimu mzima kutokana na kuendelea kutibu majeraha ya goti ambayo aliyapata kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Biashara United, Uwanja wa Mkapa.

Kwa sasa Simba ipo kwenye maandalizi ya dabi dhidi ya Yanga inayotarajiwa kuchezwa Novemba 7 baada ya ile ya awali kuyeyuka Oktoba 18 kwa hali ilivyo ni wazi kuwa Fraga ataukosa mchezo huo.

Kwenye mchezo huo wa kwanza kwa Simba msimu wa 2020/21 kucheza ndani ya Dar baada ya kuanza kufungua mkoani Mbeya kwenye ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Ihefu, Uwanja wa Sokoine.

 Fraga aliumia dakika tatu ya kipindi na nafasi yake ilichukuliwa na Said Ndemla dakika ya 8.


Kwa sasa ameendelea kufanya mazoezi mepesi ili kurejea kwenye ubora wake lakini kurejea uwanjani inatajwa itamchukua muda mrefu.


Kocha Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck amesema kuwa anasikitika kukosa huduma ya kiungo huyo ambaye alikuwa anatimiza majukumu yake kwa umakini ndani ya uwanja.


"Kuhusu Fraga ninasikitika kwamba atakuwa nje kwa muda wa miezi sita, hivyo sitakuwa naye kwa msimu mzima hili ni jambo la huzuni.


"Kikubwa ni kuona kwamba anaweza kupona na kurejea kwenye majukumu yake ndani ya timu," amesema."

1 COMMENTS:

  1. Nampa pole, kama ni hivyo nafasi yake basi asajiliwe yule winga wa UDSONGO (king) kahata asiachwe; Pia nashauri iongezwe jezi ya nne ya Simba SC ambayo itakuwa na Rangi ya ngozi ya simba mnyama itatumika katika mazoezi n.k; mazingira ambayo yataakisi hali halisi ya jina la simba SC na kumtangaza mnyama huyo hatari aliyepo katika mbuga zetu za taifa.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic