KATI ya wachezaji mahiri zaidi kwenye Ligi Kuu ya Hispania, La Liga yupo mshambuliaji wa Real Madrid, Karim Benzema. Madrid imekuwa na wachezaji wengi sana mahiri na alipoondoka mshambuliaji Cristiano Ronaldo iliaminika kuwa timu hiyo itayumba.
Hata hivyo, pamoja na kuondoka staa huyo bado Benzema ameonekana kuwa kwenye chati ya juu sana pamoja na kwamba hapewi sifa inayostahili.
Benzema amecheza Real Madrid kwa kipindi kirefu na amefanikiwa kupata makombe kadhaa akiwa na timu hiyo na ni mmoja kati ya washambuliaji waliokaa kwenye timu hiyo kwa muda mrefu.
CHINI NI TAKWIMU ZA STAA HUYO KWENYE KIKOSI CHA MADRID;
Umri: Miaka 32
Misimu aliyokaa Real: 11
Mabao aliyofunga Real: 255
Michezo aliyocheza Real: 524
Wastani wa mabao kwa msimu: 20
Makombe aliyotwaa Real: 18
Makombe la Liga: 3
Makombe ligi ya Mabingwa: 4
Jumla ya timu alizochezea: 2
Jumla ya mechi zote: 692
Jumla ya mabao: 336
Michezo timu ya Taifa: 81
Mabao timu ya Taifa: 27
Kweli benzema mfalme pale
ReplyDeleteOndoa picha ya Gareth Bale weka picha ya Karim Benzema
ReplyDeleteHawa wandishi njaa huyo Ni Benzema?.Bale hata hayupo Madrid,copy and paste
ReplyDeleteAhahaha habari ina muhusu Benzema, picha Bale duh hii kali
ReplyDelete