November 5, 2020


 NYOTA wa zamani wa Klabu ya Yanga, Malimi Busungu ambaye aliwika sana na kikosi hicho mara baada ya kusajiliwa amesema kuwa kwa sasa anafanya shughuli za kilimo na ufugaji ili kuyatafuta mafanikio.

 

Awali, Busungu alitua Yanga mnamo mwaka 2015 akitokea Mgambo JKT ambapo ni miongoni mwa nyota ambao usajili wao ulitikisa kufuatia kugombaniwa na vigogo wawili, Simba na Yanga ambapo mwisho wa mchezo akatua Jangwani kwa mkataba wa miaka miwili.

 

Mshambuliaji huyo hakuweza kutamba sana katika soka la Bongo ambapo awali alianza kuzitumikia timu za Polisi Moro, Villa Squad, Coastal Union, Kagera Sugar, Mgambo JKT, Yanga na baadaye Lipuli.

 

Busungu ambaye aliitumikia Yanga kwa misimu miwili, alitimka katika kikosi hicho mwaka 2017 baada ya kuitumikia kwa misimu miwili na kujiunga Lipuli ya Iringa ambapo ndipo alipokwenda kumalizia maisha yake ya soka


Nyota huyo amesema kuwa kwa sasa anajishugulisha na masuala ya kilimo jambo lnalomfanya aendelee kuendesha maisha yake ya kila siku.


“Nimeanza kwa kujishughulisha na kilimo cha vitunguu huku Bariadi (mji uliopo mkoani Simiyu), mradi ambao naona unanilipa kwa kiasi fulani kutokana na jinsi ninavyoyaona matokeo.


“Kilimo cha vitunguu ni miongoni mwa kilimo bora hasa msimu ukiwa mzuri kwani kila msimu una mabadiliko yake na bei hupanda kulingana na msimu husika.

 

“Baada ya kutoka kwenye mpira ndiyo nikaamua kugeukia huku, sina muda mrefu na sitegemei kuachana na kilimo hiki na kwa sasa nipo katika harakati za kutafuta manufaa ya kilimo cha vitunguu,"

amesema. 


3 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic