November 5, 2020


LIGENDI wa Argentina, Diego Maradona, amefanyiwa upasuaji wa ubongo huko La Plata Buenos Aires ambapo kwa mujibu wa daktari wake upasuaji huo umefanikiwa na anaendelea vizuri.

 

Awali alipelekwa hospitali kwa shida ya upungufu wa damu na baadaye kugundulika kuwa na tatizo kwenye ubongo wake.

 

Maradona ambaye aliiongoza Argentina kushinda Kombe la Dunia mwaka  1986, atakuwa anatimiza umri wa miaka 60 ifikapo Novemba 6, mwaka huu.

 

Nyota huyo aliyechezea vilabu mbalimbali duniani, anakumbukwa sana na Waingereza baada ya kuwafunga goli akitumia mkono kwenye ushindi wa 2-1 kwenye Kombe la Dunia mwaka 1986.


Awali ilikuwa inatajwa kuwa huenda akawa anasumbuliwa na Virusi vya Corona kabla ya kufanyiwa vipimo kutokana na hali yake kubadilika ghafla.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic