November 21, 2020

 


Anaandika Hamisi Kigwangalla

 NILIKUTANISHWA na Mohammed Dewji na baba yake, Mzee GMD. Kipindi hicho tuki-supply MeTL marobota ya pamba kutoka kiwandani kwetu.

 Alikuwa Mbunge wa Singida Mjini na mimi nikiwa nafanyia kazi ndoto zangu za kuingia bungeni. Kuanzia hapo tulikutana mara nyingi, zaidi kibiashara. Mwaka 2010 sote tulibahatika kuingia bungeni.

 Tulijenga urafiki na kushirikiana mambo mengi. Tuliunganishwa na mambo mengi; upenzi wa Simba, siasa na ujasiriamali. Kwa mahusiano/historia hii haikuwa tabu kumwomba mkopo wa pikipiki, tena wa mwezi mmoja tu.

 Mimi kama mkulima/mfanyabiashara ya mazao, ninakuwa na ‘stock’ ambayo huuza bei zikichangamka. Na yeye si mgeni kwenye hili. Ndiyo biashara. Kwa kuwa yeye ni jamaa yangu na ana stock ya pikipiki, kuniazima haliwezi kuwa jambo zito saaana, kama naweza kuweka dhamana.

 Wapiganaji mjini tunafanya sana hii. Kwa wale maskini wenzangu, kukopa ni upiganaji unaosaidia kufanikisha jambo na wala siyo jambo la aibu, kimsingi ni harakati ya kupambana na umaskini. Kama hujawahi kukopa, basi haujapigana ipasavyo, ongeza bidii! 

Inawezekana nilihoji maswali magumu juu ya mustakabali wa ‘transaction’ ya Simba. Inawezekana nilimkera jamaa yangu. Lakini hakupaswa kwanza kutoa ‘Siri’ za kibiashara hadharani, jambo lililolenga kunidhalilisha, pili kuitumia hii situation kutoa majibu ya maswali ya msingi niliyouliza.

 Kunidhalilisha na kunichafua, nilijua tu ingekuwa ni ‘quick fix’ ya muda tu, isingesaidia lolote, sababu nilijua kuna mambo mengi ya msingi hayakuwa sawa kwenye ‘transaction’ yote. Wanasimba tunataka ushindi dakika 90 uwanjani na mchango wa Mohammed siyo wa kudharau kwenye hili, lakini hata yeye na biashara zake wanafaidika na Simba as a brand, siyo bure tu.

 Thamani ya Simba siyo majengo, ni brand yenye umri wa zaidi ya miaka 80. Tanzania ni lazima uwe Simba ama wale wengine...hata kama unamiliki timu yako. Siyo kitu kidogo. Simba ina maslahi ya umma. 

Ninaweza kusema mengi lakini siyo lengo langu. Nimekuwa nikiwaza juu ya kusameheana. Yaishe. Tusonge mbele. Naomba radhi kwake na kwa washabiki wote wa Simba niliowakwaza. Mimi nimesamehe. Maisha yaendelee. #HK #NguvuMoja

10 COMMENTS:

  1. Unajua mtu unapotafuta kiki matokeo yake ikabuma kifuatacho ni aibu

    ReplyDelete
  2. Kiki????? Wapi! Ilikuwa akiongea sawa na alichokuwa akikiongea ndio hicho ambacho boss mo mpaka sasa ameshindwa kukikamilisha na ndio kimechelewesha mchakato wa mabadiliko ya uwekezaji ndani ya Simba.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ww umeweka shilingi ngapi Simba usiropoke tu.

      Delete
  3. Bravo Hamis Kigwangala Kwa busara uliyotumia ya kuomba kusameheana.Kwa wana SIMBA hatuna budi kusonga mbele na kugangaa na yajayo kwani sote dhamira yetu ni kuijenga Simba imara hivyo hakuna haja ya kugombania fito wakati wote tunajenga nyumba moja.Yote kheri...InshaAllah.

    ReplyDelete
  4. The weak can never forgive, while Forgiveness is the tribute of the strong. Hatred can never drive out hatred, only love can do that.

    ReplyDelete
  5. Msingi mkubwa wa andiko la Hamisi umejikita kwenye kumnanga MO kutokana na lile sakata la bodaboda na wala sio kumuomba msamaha,ukisoma andiko lote utaona asilimia kubwa ya mwili wa ujumbe ni kukumbushia lile suala na hili limekuja baada ya kuibuka malumbano kati ya MO Simba na FCC sasa jamaa amechukua opportunity kugongelea msumari.Inabidi utumie akili na busara kidogo kutafakari na kulielewa andiko.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Na huo ndiyo ukweli. Ujanja wala hila hautalimaliza hili. Sasa hao FCC nao walimuomba mkopo au posho? Unaweza ficha nundu lkn sio mapembe. Mchakato wa ubinafsishaji wa Simba hauko sawa na ndio maana hauendi mbele. Mo aliwahi kuimilki African Lyon na Singida United z (Mto) kwa nini aliziacha? Na kwa nini haiachii Simba, ni kwa kuwa Simba siyo majengo, viwanja na mahesabu yaliyokaguliwa tu; nembo ya Simba ina Social, Market na Financial values.
      Nembo ya Simba kaibadili (eti Simba wa zamani ni mwoga), jezi na nyaraka zote za Simba zinatangaza bidhaa za Mohammed Enterprise kwa gharama ipi?
      Najua msiopenda panadol mtanibarasa sasa hivi lkn ukweli ndo huo.
      Nazima data

      Delete
    2. Ukiwasha data elewa siku zote dua la kuku halimpati mwewe na acha kuwa na wivu wa kike.Iko siku MO na Simba watafanikisha tu na yote kheri..Insha'Allah.

      Delete
  6. Huo ni uelewa waking Latina tuuheshimu kama tunavyoheshimu mawazo ya watu wengine. Ametambua kosa lake ndo maana kaamua kuomba msamaha yaishe na tusonge mbele maana malumb hayajengi zaidi ya kubomoa tu.

    ReplyDelete
  7. Nawe pia ungekuwa muungwana kama ungemfata inbox kishkaji kama unavodai ni jamaa yako ukamhoji huko, ulikuwa na maana gani kuhoji mitandaoni, huoni hivo kwamba unajenga picha kwamba baada ya kunyimwa pikipiki ndo ukaamua kuhoji mitandaoni?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic