November 21, 2020

 


MEDDIE Kagere na Luis Miquissone wawili hawa wanatarajiwa kukosa mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Coastal Union utakaochezwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.

Kagere raia wa Rwanda na Luis wa Msumbiji wamekuwa na pacha nzuri uwanjani ambapo kwa pamoja wamehusika kwenye mabao 12 kati ya 22 yaliyofungwa na Simba.

Kagere amefunga mabao manne na Luis amefunga bao moja na kutoa jumla ya pasi sita za mabao ndani ya msimu wa 2020/21. 


Mchezo wa leo utakuwa wa kwanza kwa Coastal Union kukutana na Simba kwa msimu wa 2020/21 jijini Arusha.


Kwa mujibu wa Meneja wa Simba, Abbas Ally,'Gazza' amesema kuwa wawili hao wamechelewa kujiunga na timu kwa kuwa walikuwa na majukumu kwenye timu zao za Taifa.


"Tunatarajia kukosa huduma za wachezaji wawili Meddie Kagere na Luis Miquissone ambao walikuwa kwenye majukumu yao kwenye timu zao za Taifa, " amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic