November 22, 2020


YANGA ikiwa Uwanja wa Mkapa imegawana pointi mojamoja na Namungo FC ya Lindi kwenye mchezo wa ligi raundi ya 11. 

Bigirimana Blaise, leo Novemba 22 amemwaga machozi baada ya dakika 90 kukamilika kutokana na kitendo cha kukosa penalti dakika ya 90 baada ya kipa namba moja wa Yanga kuiokoa kwa kuitema na aliporudia mara ya pili alipaisha mpira huo mazima.


Yanga ikiwa Uwanja wa Mkapa imelazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Namungo kwenye mchezo uliokuwa na ushindani mkubwa mwanzo mwisho.


Mabao ya timu zote mbili yalipatikana kipindi cha kwanza ambapo Carlos Carlinhos alifunga bao la kwanza kwa Yanga dakika ya 13 kwa pasi ya Kibwana Shomari na dakika ya 16, Stephen Sey alipachika bao la kusawazisha kwa guu la kushoto.


Penalti ya Blaise iliyopaishwa ilipatikana dakika ya 90 baada ya beki,Bakari Mwamnyeto kumchezea faulo kiungo Shiza Kichuya ndani ya 18 na alionyeshwa kadi ya njano.


Mvutano mkubwa ilikuwa ni nani ambaye angepiga penalti hiyo jukumu likawa la Blaise mwenye mabao manne ambaye alikosa penalti hiyo baada ya Mnata kumsoma kwa umakini na kuipangua jumlajumla.


Sare hiyo inaifanya Yanga kugawana pointi mojamoja na Namungo FC Uwanja wa Mkapa huku Mnata akipewa zawadi ya noti na mashabiki baada ya kutimiza majukumu yake kwa umakini.


Yanga inafikisha jumla ya pointi 25 sawa na Azam FC ambayo ipo kileleni kwa idadi ya mabao huku Namungo ikibaki nafasi ya 9 na pointi zake ni 15.

4 COMMENTS:

  1. Yanga ikitoka droo na Azam na Simba kuifunga Katika mchezo ujao basi Mmyama anashika usukani kutokana na gunia lake tele la magoli. Gongowazi hawakuwa wakijitambuwa Katika mchezo wa Jana na walikuwa ovyo

    ReplyDelete
    Replies
    1. Watabiri vipi huko Nigeria hawaendi tena?

      Delete
    2. Mfuasi wa TB Joshua tupe utabiri wako dhidi ya mechi ya Plateau

      Delete
  2. Watapata tabu Sana yanga Simba mbele tu Sasa ndio watajua faida ya magoli mengi si wanasema wao kikubwa point tatu Sasa ukikutana na team yenye mastraika wazuri hawatakosa kukufunga zaidi ya Gori moja mrundi Blaise umeigharimu team kwa tamaa ya kuongeza magori ulionekana kabisa hukuwa mchezoni ungemwachia kichuya au Lucas kikoti Tena hata awamu ya pili ukakosa Tena

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic