December 14, 2020


 IMEELEZWA kuwa uongozi wa Mwadui FC umemfuta kazi Kocha Mkuu wa timu hiyo Khalid Adam kutokana na mwendo mbovu wa timu yake.


Adam amekiongoza kikosi cha Mwadui FC kwa msimu wa 2020/21 ndani ya Ligi Kuu Bara kwenye jumla ya mechi 15 na imeshinda mchezo mmoja pekee ndani ya ligi.


Mechi 11 amepoteza na kuambulia sare moja huku timu hiyo ikiwa nafasi ya 18 baada ya kukusanya pointi 10.


Mchezo wake wa mwisho kukaa benchi ilikuwa Desemba 12 ambapo alipokea kichapo cha mabao 5-0 dhidi ya Yanga ikiwa ni ushindi mkubwa kwa Yanga inayonolewa na Cedric Kaze kwa msimu huu.


Akizungumza na Saleh Jembe, Meneja wa Mwadui FC David Chakala amesema kuwa bado hajapata taarifa rasmi kuhusu kufutwa kazi kwa Adam hivyo hawezi kutoa taarifa rasmi.


"Leo hatukuwa na mazoezi kwa sababu hatukuwa na mechi ila kesho ndo itakuwa siku ya kuanza mazoezi kwa ajili ya maandalizi ya mechi zetu zijazo za ligi.


"Mwalimu nimemuona hapa ila hakuwa na timu kwa kuwa hakukuwa na mazoezi labda mpaka kesho nikipata taarifa nitajua ni nini ninaweza kuzungumzia ikiwa kutakuwa na taarifa nyingine," .

7 COMMENTS:

  1. Kocha wa Azam alifungwa na yanga akafutwa kazi, kocha wa mwadui kafungwa na yanga kafutwa kazi. Ina maana timu haziamini kufungwa na yanga? Au kuna namna? Nauliza tuu msitoe mapovu

    ReplyDelete
  2. Mbwana Makata na Kaywila jiandaeni mkishindwa kuisimamisha Yanga Bye Bye. Azam walifungwa na Mtibwa wakachukulia poa tu kufungwa na Yanga ikawa nongwa. Mwadui wamefungwa weeee Ila kufungwa na Yanga tu Nongwa. Vipi ?

    ReplyDelete
  3. hapo mwandishi unatambua bak 5-0 za Yanga.Unasahau kabla ya Mwadui kukutana na Yanga ilishafungwa mabao kama hayo na JKT, KMC na Simba..kama kweli Yanga ina kawaida ya kufunga timu bao 5, tutajua mbele ya safari..
    Ukweli ni kwamba tofauti na kuwa na kikosi cha bil karibu 2, hamna kutembeza bakuli Yanga ya mwaka huu haina tofauti sana na ya Zahera mwaka juzi..Hadi ngwe ya pili mwishoni waliongoza ligi na ubingwa ukachukuliwa na mwingine.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Jifurahishe na jifariji kwa historia.

      Delete
    2. bahati nzuri Malinzi hayupo tena kuwaokoa mabingwa wa kihistoria..ukweli ni kuwa ubingwa na mashindano ya kimataifa imeishakuwa historia

      Delete
  4. Kweli mikia munashida Sana kwaaio kwaakiliyenu munajua ndomtakua mabingwa kilamwaka mwakahuu hatamununue mechiz
    ote yanga humuitoi kwenjia

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ropokeni tu ligi bdo mbichi, mume wenu anapambana kimataifa endeleeeni kuandaa chakula nyumbani.

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic