December 26, 2020


 

 IBRAHIM Ame beki wa kati ndani ya kikosi cha Simba huenda akarejea ndani ya timu yake ya zamani ya Coastal Union kwa mkopo ili kuongeza makali yake baada ya kujenga ushkaji na benchi.

 

Habari zinaeleza kuwa miongoni mwa majina wa nyota watakaotolewa kwa mkopo kwenye dirisha la usajili dogo ambalo limefunguliwa Desemba 16.

 

Kocha Mkuu wa Coastal Union,  Juma Mgunda anahitaji kuboresha safu ya ulinzi ambayo imekuwa ikipata tabu baada ya nyota wake wawili kusepa ikiwa ni pamoja na Bakari Mwamnyeto ambaye yupo Yanga.

 

Hivyo kutokana na ugumu anaoupata Ame ndani ya Simba mabosi Coastal Union wamefikiria kuipata saini ya beki huyo mzawa mwenye uwezo ndani ya uwanja.

Coastal Union kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara ipo nafasi ya 13 na pointi zake ni 19 kibindoni.


Safu yake ya ushambuliaji imeokota nyavuni jumla ya mabao 21 baada ya kucheza jumla ya mechi 17.

5 COMMENTS:

  1. Kwani ame anashida gani zaidi ya simba kutomtumia.hakuna mechi amecheza akashindwa kufanya vizuri kama ni kweli nadhani simba wameshindwa wenyewe kumtumia na kumwamini wasisingizie kukuza kiwango

    ReplyDelete
  2. Acha kusikiliza wauza magazeti

    ReplyDelete
  3. Kusajili kwa pupa kwa hizi timu za bongo hasa SIMBA na YANGA kwakwel kuna haribu vipaji vya wachezaji

    ReplyDelete
  4. Hilo litakuwa kosa la mwaka. Pale simba mabeki wote wazee, wapeni vijana nafasi waonyeshe ujuzi wao

    ReplyDelete
  5. Amee na usajili wake wA kuwatime Yanga??????!!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic