December 26, 2020

 


MWENYEKITI wa zamani wa Klabu ya Simba, Ismail Aden Rage amefunguka kuwa Yanga kuendelea kung’ang’ania suala la Morrison kwenye Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS) ni sawa na kupoteza muda kwani hakuna chochote ambacho watapata kwenye kesi hiyo.

 

Rage alikwenda mbali kwa kusema kuwa hakuna sheria yoyote inayosema mshitaki na mshitakiwa wote wanatakiwa kulipia fedha ili kesi yao iweze kusikilizwa na CAS kama ambavyo taarifa ya Yanga ilivyosema wao na Morrison wanatakiwa kuchangia fedha za Kifaransa ‘Franc’ 24,000 kwa maana ya kila mmoja kuchangia Franc 12,000 (zaidi ya Sh milioni 5).

 

Akizungumza na Championi Jumamosi, Rage alisisitiza kuwa: “Kama kweli wametumiwa hiyo barua na CAS ya kulipia hizo fedha waambie wakuonyeshe hizo karatasi, hakuna kitu kama hicho kwamba mshitakiwa na mshitaki wanatakiwa kulipa ada ya kesi yao kusikilizwa. Wanachofanya Yanga ni kupoteza muda tu, hawatapata chochote.


"Nikwambie kuwa kesi zote za CAS zitasikilizwa Januari 12, chukua maneno yangu kesi zote zilizopo CAS zitasikilizwa na hakutakuwa na kesi ya Morrison na Yanga,” alisema Rage.

 

Klabu ya Yanga kupitia kwa Makamu Mwenyekiti wake, Frederick Mwakalebela alisema kuwa wametumiwa barua na CAS wakitaarifiwa kuwa jaji wa kusikiliza shauri lao la kimkataba na Morrison amepatikana na watatakiwa kulipia kiasi hicho cha fedha kabla ya Januari 12, mwakani ili kesi iweze kusikilizwa.

 

Yanga walikata rufaa na shauri lao kulipeleka CAS mara baada ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kubaini upungufu kadhaa kwenye mkataba wa Morrison ambao alipewa na Yanga, na hadi wakati kesi yake ikiendelea tayari alikuwa amesaini Simba.

20 COMMENTS:

  1. Haha hizi drama ila kuna propaganda Zach kimechezo hasa ktk psychology.....

    ReplyDelete
  2. Kuna viongozi utendaji wao unatia shaka, wanachokiweza ni kufurahisha mashabiki pasipo manufaa yoyote

    ReplyDelete
  3. Wewe rage tulia unaumia nini?

    ReplyDelete
  4. Mimi nilisema pia, hakuna utaratibu wowote unamtaka mshitakiwa alipie kikao cha kesi, huo ji ujinga, kama nikikataa? Viongozi wa yanga wanawafanya washabiki wao kama vile hawawezi kufikiri. Hili suala morrison walipotezee, vinginevyo litawaingiza matatani. Wasijifanye hawajui kuwa walifoji moataba na TFF wakaamua kiutu uzima kuzima soo.

    ReplyDelete
  5. Uyo rage ni mpuuzi tu INA maana anataka kujifanya yeye ndo anawazidi akili viongoz wote kwnye suala la taratibu? Anajaribu kukwepesha mambo kishabiki sasa ngoja tusubili tuone kama aitosikilizwa, na akawaambie simba wamchezeshe uyo mchezaji basi kama wana ubavu si anasema akuna kesi?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kiongozi kasema Mshtaki na mshtakiwa wachangie ili kesi iendeshwe, mmoja wapo asipochangia kesi inafutwa. Hivi hii inakuingia akilini kabisa

      Delete
  6. Kwan Morison.hachezi Simba?ujue Kuna watu cjui wqnafikiri kutumia kiungo gan yan hajawah kumuona Morison.akiitumikia clab y Simba

    ReplyDelete
  7. Huu uandishi wa namna hii ni upotoshaji wa hali ya juu sana.yaani maoni ya mwenyekiti wa zamani ndiyo tafsiri ya tamko la simba?

    ReplyDelete
  8. Huu uandishi wa namna hii ni upotoshaji wa hali ya juu sana.yaani maoni ya mwenyekiti wa zamani ndiyo tafsiri ya tamko la simba?

    ReplyDelete
  9. Hapo ndio tuna uvilaza wa waandishi wetu wanaandika bila kupata uthibitisho leo lanatoa story ya uongo kesho wanatoa story ya kukanusha ili mradi wauze magazeti

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mtuoneshe hyo barua siyo kelele tu, GSM na viongozi wenu wanaendelea kuwachezeachezea nanyi mashabiki utopolo mfurahia kuchezewachezewa.

      Delete
  10. Rage naye kuma tu Kwan sheria kasomea wapi! Kitaluma yule siyo mwanasheria kwahiyo anawapotosha nguruwe fc wenzake ili wasiulizie billion 20 na wasiulize kwa nn MORRISON hachezi?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hii utopolo nahc imelaniwa, samahani kwakutumia maneno makali bila tafsida, matukio mabaya yote utopolo kwasehemu kubwa. Lugha chafu-utopolo,uhongaji-utopolo,ubaniaji wa riziki ya wachezaji- utopolo n.k

      Delete
    2. Ugomvi uwanjani-utopolo *kupiga mashabiki wa team pinzani*, viongozi na mashabiki mbumbu wengi wasiyojua mpira unahitaji kitu gn wanatoka utopolo

      Delete
  11. Matusi ya nini sasa, uwe na adabu hata kama hupendi kilichosemwa. Mtu mzima unatukama matusi mazito bila sababu ya msingi, aibu sana.

    ReplyDelete
  12. Rage ?Jana mlimponda leo ananukuliwa Ila kwangu Mimi huwa namwona mpiga propaganda kesi za mpira ni utapeli tu, kwanini mikia hawachezi Ligi? au mnataka kusajili namba 10 Sassi mwingine,na kifuatacho Kuna joke refa Zabron utashangaa anaanza kupangwa Saidia Simba .mcheze mpira huyo Msomali Karia anataka kutuharibia Ligi tutamwambia Bashungwa uzuri naye Mwananchi

    ReplyDelete
  13. Sasa hivi yanga wameambiwa na fifa walimpeHamis Tambwe milioni46 na wamepewa siku 45 wasipolipa watafungiwa kusajili lakini wamekwepa kuzungumzia ila ya Kichuya walikimbilia kuandika haraka

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hao👆 utopolo wanataka Kiki kupitia morrisoni wakati wenzao wanajitangaza uwanjani.
      Viongozi wao wakili tu waliingia Chaka kwenye mkataba wa morrison.
      Tafakarini hata mtoto anayesoma vidudu anawazidi hesabu

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic