December 16, 2020

 


FRANCIS Baraza, Kocha Mkuu wa Biashara United amesema kuwa atasajili washambuliaji wawili ndani ya kikosi chake ili kuongeza makali kwenye kikosi hicho.

Ikiwa imecheza jumla ya mechi 15, safu yake ya ushambuliaji imefunga jumla ya mabao nane na kinara ni Kelvin Friday mwenye mabao mawili.

Safu yake ya ushambuliaji imeruhusu mabao ya kufungwa 16 ikiwa nafasi ya 8 na pointi zake kibindoni ni 20.Habari zinaeleza kuwa timu hiyo inahitaji kupata huduma ya nyota wa Simba, Charles Ilanfya kwa mkopo.

Akizungumza na Saleh Jembe, Baraza amesema kuwa kuna kazi kubwa kwa kikosi chake kufanyiwa maboresho hasa safu ya ushambuliaji.

“Kwangu mimi naona kwamba ligi ina ushindani mkubwa, kikosi changu tatizo lake ni moja kwenye umaliziaji wa nafasi tunazotegeneza. Kutokana na jambo hilo ni lazima tuongeze washambuliaji wawili.

“Tukipata washambuliaji hao kazi itakuwa imekwisha kwa upande wa tatizo la ufungaji tutahamia kwa mabeki, ila wote tutawachukua wale wenye uwezo na uzoefu,” amesema Baraza.


Miongoni mwa nyota ambao wanatajwa kuingia anga za Biashara United ni Ilanfya mshambuliaji wa Simba ambaye hana nafasi kikosi cha kwanza pamoja na Marcel Kaheza wa Polisi Tanzania.

3 COMMENTS:

  1. Acheni kuzingua!mechi ya tatu ya Simba hamtuwekei kikosi kinachocheza..wakati utopolo wakicheza hata na Stendi United masaa kabla ya mechi mnaweka kikosi uto..nyie wa ajabu kweli.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kikosi utakipata kwenye matangazo ya radio au ya Tv unaweza kusoma kikosi humu kumbe sio chenyewe maana hawa jamaa zetu hawaaminiki

      Delete
  2. Roho zinamauma. Simba ameshinda.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic