December 16, 2020


KIPA namba mbili wa Yanga Faroukh Shikhalo raia wa Kenya huenda akaachwa kwenye usajili wa dirisha dogo ili ampishe kiungo mchezeshaji wa kimataifa katika kukiimarisha kikosi hicho.

 

Dirisha la usajili limefunguliwa Desemba 15, mwaka huu huku timu hiyo ikiwa tayari imekamilisha usajili wa kiungo mshambuliaji, Mrundi, Said Ntibazonkiza ‘Saido’.

 

Yanga imepanga kufanya usajili wa wachezaji watatu kati ya hao wapo wazawa na kimataifa waliokuwepo kwenye mazungumzo ya mwisho na timu hiyo na kiungo anayetajwa kutua Yanga ni Isah Ndala anayekipiga Plateau United ya nchini Nigeria.

 

Habari zimeeleza kuwa Yanga imepanga kuachana na Shikalo ili wapate nafasi ya mchezaji wa kigeni atakayejiunga na timu hiyo.


Mtoa taarifa huyo amesema kuwa, Yanga itaachana na kipa huyo baada ya kushindwa kuonyesha ushindani mbele ya kipa namba moja wa timu hiyo, Metacha Mnata aliyekuwepo kwenye kikosi cha Taifa Stars.

 

Aliongeza kuwa, wakijiandaa kuachana na Shikhalo, upo uwezekano mkubwa wa timu hiyo kumsajili kipa mwingine atakayempa changamoto Metacha na Ramadhani Kabwili.

 

"Yanga imepanga kufanya mabadiliko kidogo ya usajili katika dirisha dogo na wamepanga kusajili wachezaji watatu pekee kati ya hao wapo viungo na mabeki watakaojiunga na timu katika msimu huu.

 

“Hiyo ni baada ya kocha kufanya mapendekezo ya usajili wa wachezaji wapya na wale watakaowatoa kwa mkopo na kuachana nao jumla baada ya kushindwa kuonyesha ushindani katika timu.

 

"Kati ya wachezaji ambao huenda wakaachwa ni Shikalo ambaye yeye amekosa nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza na kujikuta akikalishwa benchi na Metacha.

 

"Hivyo mabosi wake huenda wakaachana naye ili wapate nafasi ya usajili ya mchezaji wa kimataifa, Shikalo ni kipa mzuri lakini ameshindwa kumpa upinzani Metacha,” alisema mtoa taarifa huyo.

 

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili na Mashindano wa Yanga, Injinia Hersi Said, hivi karibuni alisema kuwa: “Jukumu la usajili lote lipo chini ya Kocha Kaze (Cedric) ambaye atatoa mapendekezo ya wachezaji anaowahitaji na atakaowaacha.”

 

Kwa upande wa Kaze yeye alisema kwa hivi sasa akili yake ameielekeza katika kumalizia michezo waliyoibakisha ya Ligi Kuu Bara kwa lengo la kumaliza mzunguko wa kwanza wakiwa kileleni.


Chanzo: Championi

11 COMMENTS:

  1. Si kweli kabisa hawawez muacha Shikalo hata kwa bahat mbaya kwa kuwa hakuna goal keeper namba 2 . Achen uzush wa kupika taarifa

    ReplyDelete
  2. Yaani umuache golikipa kisha usajili kiungo...inaingia akilini kweli? Za kudanganywa changanya na za kwako

    ReplyDelete
  3. Na zaidi huone Vita ya Mo energy Yanga bado ina nafasi ya Mchezaji mmoja was Kimataifa,hapa scout ya Yanga Mwandishi itakutesa Tena sana ,nayo utashangaa kuona Saidio mwingine ,hiyo ndala au viatu wazuge Azam
    Nq

    ReplyDelete
  4. Bado tuna nafasi moja Kama Shikalo hafai atatafutwa Kipa mwingine bt siyo kuacha cse tuna nafasi moja pending.

    ReplyDelete
  5. Na zaidi mbona wazee was vijiwe utwambii wanamwacha Nani ,najua hutaki ku demololize focus ya Simba bt ukweli pia hata Yanga wanajua Nini unaandika ,kimbunga hiki Cha ushindi hakina Kingo.
    E

    ReplyDelete
  6. mechi ya tatu ya Simba hamtuwekei kikosi kinachocheza..wakati utopolo wakicheza hata na Stendi United masaa kabla ya mechi mnaweka kikosi uto

    ReplyDelete
  7. Mmeanza sasa kutumiwa ili mtuvuruge acheni huu ujinga wenu...haachwi mtu

    ReplyDelete
  8. Shikalo ndio kipa mwenye footwork nzuri kwa modern football aiingi akilini kabisa kumuacha na haitatokea angalia pasi yake iliyozaa goli Singida ndio utamjua alafu angalia alichofanya Kakolanya ndio utajua hamna footwork pale ni miguu ya kutembelea tu -:)))))

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hawa waandish hawana jambo la kuandika ndio maana wanapika story. Kaze amekanusha kumuacha Shikalo. Wao hizi habar za kuachwa kwake wanazipata wapi?

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic