December 24, 2020


 BODI ya Wakurugenzi ya Klabu ya Simba, imesitisha mipango ya kumsajili kiungo mkabaji wa Plateau United ya nchini Nigeria, Isah Ndala. Hiyo ikiwa ni siku chache tangu wakamilishe usajili wa kiungo raia wa Uganda, Taddeo Lwanga.


Lwanga amesaini dili la miaka miwili ndani ya Simba na amepewa mikoba ya nyota Gerson Fraga raia wa Brazil ambaye anaendelea kutibu jeraha lake la goti.

 

Simba katika usajili huu wa dirisha dogo uliofunguliwa Desemba 16, mwaka huu, Ndala alikuwepo kwenye mipango yao.


 Nyota huyo aliisumbua safu ya kiungo ya Simba wakati walipocheza dhidi ya Plateau kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.

  

Kaimu Mwenyekiti wa Simba, Mwina Kaduguda amesema kuwa timu hiyo haitasajili kiungo mwingine mara baada ya kukamilisha usajili wa Lwanga.

 

Kaduguda amesema kuwa wamepanga kusajili wachezaji wawili pekee ambao ni beki wa kati na mshambuliaji namba tisa pekee.

 

“Ilikuwepo mipango ya kumsajili Ndala lakini hivi sasa haipo tena kwani tayari tumemsajili Lwanga anayecheza nafasi hiyo,” amesema Kaduguda.


Lwanga ambaye ni kiungo mkabaji alikwama jana  kucheza kwenye mchezo wa kimataifa dhidi ya FC Platinum kutokana na vibali vyake kuchelewa kufika.


Simba ilinyooshwa kwa bao 1-0 dhidi ya FC Platinum inatarajiwa kurejea nao Januari 6, Uwanja wa Mkapa.

3 COMMENTS:

  1. Mmeishiwa cha kuandika nyie

    ReplyDelete
  2. Usajili ji tatizo simba.
    Lawama zote anasukumiwa kocha hii si sawa timu inasajili wachezaji wa kawaida wakija kimataifa wanashangaa tu. Simba imekuwa ya kudhibitiwa kirahisi na wapinzani kwa kuwa inaundwa na wachezaji wachache kadhaa wenye kuibeba timu na ikitokezea timu pinzani kuwadhibiti hao wachezaji timu nzima ina paralyze. Wachezaji wote wanatakiwa kuibeba timu sio chama au Miquisone peke yao. Na ndio maana watu wana shauri simba piga ua lazima wasajili kiungo mchezeshaji mwenye nguzu zaidi anaecheza tofauti na chama kuja kuipa nguvu timu kama chama atakamatwa na wachezaji wa timu pinzani. This is Simba bana tutashindwaje na utopolo kwenye usajili timu ambayo haishiriki hata kombe la kugombania Pweza. Simba is champion league team but we have problem of recruiting successful champion league players.Hatuwezi kuwa cheap kwenye usajili halafu tukawe dominant kwenye champion league hiyo ni sawa na kununua ticket ya bahati nasibu ya shilingi mia moja kutarajia kushinda million mia moja. Mafanikio hayabahatishwi lazima yafanyiwe kazi.Kwa bahati mbaya watanzania tunaamini sana bahati kuliko mikakati ya maana. Hata wachezaji wetu wanaamini sana bahati kuliko kujituma.Tutachelewa sana..mimi nafanya mazoezi kwa masaa mawili ya Gym non stop siku tatu kwa wiki si kwa ajili ya mashindano kujieka fiti tu na kuwa na muenekano mzuri wa mwili. Vijana wetu kwa maana ya wachezaji huwa wanajieka tayari kwa kiwango gani kwenye kazi zao pale kwenye pitch? Nnaimani wapo wachezaji wenye kujua thamani ya kazi zao kama si Tanzania basi nje ya Tanzania.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic