December 24, 2020


 UONGOZI wa Yanga umesema kuwa Klabu ya Yanga inaaamini kwamba haki yao ya mchezaji wao wa zamani Bernard Morrison itatendekeka kwa kuwa kesi itasikilizwa baada ya Fifa kuwapa jaji atakayesikiliza kesi hiyo.

Fredrick Mwakalebela, Makamu Mwenyekiti wa Yanga amesema kuwa Fifa imesema kuwa maelezo ambayo aliyatoa mlalamikiwa Morrison baada ya kutakiwa kufanya hivyo hayana mashiko hivyo kesi itaendelea kusikilizwa na haki itatendeka. 

Mwakalebela amesema:-"Tumepewa barua mbili na Fifa baada ya kupeleka malalamiko yetu kuhusu Morrison. Tumepokea barua ambayo inaeleza kuwa tayari tumepata jaji ambaye atasimamia kesi yetu na kila kitu kinakwenda sawa.

"Awali mlalamikiwa ambaye ni Morrison alitakiwa kuandika barua ya kutaja sababu baada ya sisi kumlalamikia Fifa ambapo sababu zake tumeambiwa kwamba hazina mashiko.

"Inatakiwa kulipa fedha kwa pande zote mbili ili kesi isikilizwe na kiasi ambacho kinatakiwa ni fedha za Kifaransa ambazo ni 12,000 jumla 24,000 mlalamikaji na mlalamikiwa anapaswa kulipa.

"Sisi tumedhamiria kulipa fedha hizo ili kesi iweze kusikilizwa na jukumu letu ni kuona kwamba haki inatendeka na kila upande una kazi ya kulipa fedha hizo na ikiwa upande mmoja utashindwa kulipa basi kesi itafutiliwa mbali," .

Morrison amekuwa kwenye mvutano na mabosi wake wa zamani Yanga ambapo kabla ya kuibukia ndani ya Simba alikuwa akiwatumikia.


Mvutano wake unatokana na ishu ya mkataba ambapo mchezaji amekuwa akisema kwamba mkataba wake ndani ya Yanga ulikuwa ni wa miezi sita huku mabosi wake wakidai kwamba alisaini dili la miaka miwili.

Mpaka anajiunga na Simba kwa kandarasi ya miaka miwili bado alikuwa kwenye mvutano ambapo kesi yake ilisikilizwa kwa muda wa siku tatu mfululizo makao makuu ya Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF).

Maamuzi ambayo yalitolewa awali yaliweka wazi kwamba mkataba wa Morrison na Yanga ulikuwa na mapungufu hivyo mchezaji huyo alipewa ruksa ya kuchagua timu ambayo anahitaji.


13 COMMENTS:

  1. Hakuna kitu hapo. Sasa mlalamikiwa anatakiwa kulipa pesa ya nini ili hali haijajulikana kama ana kesi? Maamuzi yakitoka ndio itaamuliwa gharama ya kesi nani mlipaji. Sio unanishitaki halafu unataka nikusaidie kuendesha kesi, hapo sijaelewa

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kichwa kigumu wewe kwani nimeambiwa fedha inayolipwa ni adhabu.umeambiwa ni fee ya kusikilzwa kesi acheni mahaba

      Delete
    2. hujaelewa!!!!!.....heeeh,utaelewa tu,subiri kidogo.

      Delete
    3. Mbulula kama wewe uwezi kuelewa hakuna cha bure dunia hii ndio nyie mnapigwa kesi jaji lazima alipwe na plus gharama zingine huyo fala tunae bampa tu bampa hatacheza mpira hapa tzee tena

      Delete
    4. Poleni Utopolo mnaojifanya mna vichwa vyepesi vya kuelewa haya tuambieni mmeleewa nini, mmeelewa kuwa vingozi wenu wanawaongopea ili muendelee kusherehekea kuongoza ligi kwa muda na badae muanze kusema TFF Simba teh teh teh teh

      Delete
  2. Waache waendelee kuwaongopea washabiki wao UTOPOLO fc

    ReplyDelete
  3. Eti upande mmoja ukishindwa kulipa kesi itafutwa kwahiyo morisson alipie kesi ili yanga wapate haki hiyo ni akili??

    ReplyDelete
  4. Mikia kulalama tulieni.. kama mnanyolewa. Hahaha..

    ReplyDelete
  5. Chura kwa kuongopewa na viongozi wao , si washajua akili zenu kama alivyosema Luc Eymael yani kwa kifupi ni Mnayani fc

    ReplyDelete
  6. Yanga hovyo kabisa.Mara sijui Morrison hana nidhamu arejeshwe kwao Ghana..Aa sijui Morrison hana kiwango hicho hatumuhitaji,Aa sijui Tusila zaidi ya Morrison. Sijui tena tutamsajili chama kulipa pigo la Morrison yaani ushuzi mtupu wanaweweseka. Yanga walimsaini Yondani kutoka simba kizuluma na kiujanja ujanja na simba hawakupewa haki Yao.Yanga haohao walimsaini Mbuyu twite aliekuwa keshasaini simba yaani alikuwa mchezaji halali wa simba kabisa na mambo yaliishia kienyeji kienyeji tu. Yanga wakaja kumsajili Piusi Buswita iliekuwa keshasaini simba kwa maana yakwamba alikuwa mchezaji halali wa simba na mambo yaliishia hivi hivi tu. Yanga haohao wakaja kumsaini Hasani kessy kimagumashi kwa kuvunja sheria na kanuni zote za usajili na simba hawakupata haki yao mambo yaliishia hivi hivi tu. Kwa Morrison Yanga wao wenyewe ndio waliofoji mkataba wa Morrison lakini wanalilia haki yao? Ama kweli mwizi akanyanganywa mali ya wizi halafu kesi anapeleka polisi?Lengo ni kumkomoa Morrison asicheze mpira Tanzania na kuwatoa simba kwenye reli. Hili suala la Morrison Yanga litawagharimu.Lakini pia kama vile wameanza kuingia mchecheto baada Barbara CEO wa simba kueleza kuwa wapo karibu kumkamata mchawi aliejifanya kiongozi wa simba kizani na kushughulikia suala la kichuya hadi kupelekea FIFA kuiomba radhi simba. Ninavyoona mimi Utopolo wanachohitaji ni kuchapwa tena na simba kwa mchezaji mwengine.

    ReplyDelete
  7. Akili ikiwa ndogo huwezi tafsiri jambo ila ushabiki ndio utapelekea utafsiri utakavyo mulisema yanga waongo hawajaenda fifa mbona morrison hachezi mutaamini mwishoni

    ReplyDelete
  8. Unajua siku zote nguruwe fc wanajifanya hawaelewa ila wataelewa tu hata kwa fimbo maana ni slow learners

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic