December 31, 2020

 


IMEELEZWA kuwa wadhamini wa Klabu ya Yanga, kampuni ya GSM imedhamiria kumshusha Bongo mshambuliaji wa zamani wa Klabu ya Angers ya Ufaransa, Ferebory Dore.


Nyota huyo anatajwa kuwa pacha wa Saido Ntibanzokiza ambaye ameshaingia jumlajumla kikosi cha Kwanza akiwa amecheza mechi mbili za Ligi Kuu Bara na kufunga bao moja na pasi tatu za mabao.


Jina la nyota huyo linatajwa kuwa mikononi mwa Mkurugenzi wa Uwekezaji wa GSM ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa Yanga, Hesri Said.


Habari za ndani ya Yanga zinaeleza kuwa nyota huyo tayari ameshamalizana na Yanga ni suala la muda tu kutambulishwa kwa mashabiki na wanachama wa Yanga.


Dore mzaliwa wa Congo mwenye miaka 31 kwa sasa ni mchezaji huru hivyo amejiunga na Yanga bure.


Msimu wa 2009/13 alikuwa ndani ya Klabu ya Angers na alicheza jumla ya mechi 105 na kutupia mabao 11 na alirejea tena msimu wa 2015-18 na alicheza mechi 18.


Injinia Hersi Said amesema kuwa wapo Kwenye mpango wa kumleta Bongo mshambuliaji matata ila jina lake wataliweka wazi hivi karibuni kabla ya dirisha dogo kufungwa.

13 COMMENTS:

  1. Mechi 105 magoli 11 halafu unamuita mshambuliaji matata

    ReplyDelete
    Replies
    1. unafikiri ligi aliyokuwa anacheza inafanana na ya bongo ambayo unaweza kujifungia mabao mengi?

      Delete
  2. Huyu hamna kitu, sasa kama hakuweza kufunga ujembe wake unatoka wapi ili atushawishi kuwa akija huku atafunga. Tusipokuwa makini tunageuzwa soko la wachezaji toka congo na burundi ili hali vijana wetu hawapewi kipaumbele. Majembe. Makoleo, mashoka, mapanga, duh! Utumwa unarejea huo

    ReplyDelete
    Replies
    1. Labda akija bongo ndo atafunga magoli, mshabuliaji kati ya mechi 105 anafunga mabao 11 tu!!! Afu tunamsifia kweli!!!

      Delete
  3. Tatizo wachezaji wetu hawajitumi ndiyo sababu ya hao wageni kupata majina makubwa bongo

    ReplyDelete
  4. Tujuulishwe kwanini huko Fransa ametemwa. Au kaondoka huko kwakuwa anatakiwa na yanga kwakuwa atapata hela nyingi zaidi kuliko huko Ufaeansa?

    ReplyDelete
  5. Hapo hakuna mtu ni kuuzana mtaani tu

    ReplyDelete
  6. Ashazeeka kwanza huyo,nawashauli viongozi wa yanga waachane nae (31) duh! Hiyo pesa wamtibie mapinduzi balama tu ataziba pengo la sarpong na nchimbi

    ReplyDelete
  7. We mwandishi amejiungwvna Yanga BURE?????????

    ReplyDelete
  8. GSM watasajili kila mchezaji? Mara Chama yuko mikononi mwa GSM - mara ametengewa nyumba kufuru - mara time will tell - sijui mashabaki wa timu yetu pendwa ya Yanga tuchukue lipi

    ReplyDelete
  9. Sie twahitaji ushindi tu, mengine pelekeni mikiani huko jembe letu la Ufaransa njoo.

    ReplyDelete
  10. Yanga mchezaji yeyote akija jangwani hata umri umeenda anafanyaga vyema utamfananisha na kizee onyango? acheni unafiki kwanza ishukuruni yanga kwa kuwazoesha kufata wachezaji congo yanga tunapiga tu! mwenye wivu ajinyongee miguuni afe polepole! shenzi nyinyi

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic