December 31, 2020

 


UKIWEKA kando ishu ya kuwa namba moja ndani ya Ligi Kuu Bara baada ya timu yake kucheza jumla ya mechi 17 na kibindoni kukusanya pointi 43, Cedric Kaze amewapoteza makocha wengine Bongo kwa mkwanja.


Inaelezwa kuwa Kocha Mkuu, Kaze anapokea mshahara mkubwa kuliko makocha wengine ndani ya Ligi Kuu Bara. 


Anatajwa kuvuta kiasi cha dola 10,000 (zaidi ya milioni 22) ambazo zinatolewa na mdhamini wao Bilionea Gharib Said Mohamed (GSM).


Unaambiwa hiyo ni mshahara pekee achana na marupurupu pamoja na bonasi ambazo anazipokea pale timu inaposhinda ndani ya Ligi Kuu Bara pamoja na mechi za FA ambazo bado hajaanza kucheza.


Anafuatiwa na Sven Vandenbroeck, Kocha Mkuu wa Simba ambaye inatajwa kuwa analipwa dola 9,000 sawa na milioni 20 za kibongobongo.


Chanzo: Championi

5 COMMENTS:

  1. Mishahara ni siri kati ya mwajiri na mwajiriwa, sasa hizi habari za "inatajwa" zinatoka wapi kama hakuna mhusika aliyetoa hizo taarifa hadharani? Na jee hilo linapbgeza kiwango cha soka letu au mbwembwe tuu?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Isitoshe hapo pana pande mbili, moja mwajiri yupo smart kiasi gani kwenye negotiation hali kdharika mwajiriwa. Sasa mwandishi sijuwi kalenga nini?

      Delete
  2. Mm ni shabiki wa Yanga napenda kusema sio lazima sanaa kulipwa kocha hela kubwa wakati soka letu Bado Sana kikubwa ni quality ya wachezaji inatakiwa iwe kubwa Kama Mazembe na club zingine kubwa za Africa

    ReplyDelete
  3. Issue ya malipo kwa kocha ni Siri na mwajiri wake. Naipenda chama langu la daryoung Africans

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic