December 24, 2020


 KARIM Benzema staa wa kikosi cha Real Madrid amesema kuwa atazidi kupambana ndani ya uwanja ili kufikia mafanikio ambayo anayahitaji.


Ndani ya La Liga, Benzema ni miongoni mwa wale wakali watatu wa kutupia nyavuni huku akimpoteza nyota wa Barcelona, Lionel Messi.

Benzema akiwa amecheza mechi 13 ametupia jumla ya mabao 8 na pasi tano za mabao huku akiwa amepiga jumla ya mashuti 33.

Wengine wenye mabao 8 ni Iago Aspas wa Celta Vigo na ana pasi 5 pia za mabao akiwa amecheza mechi 15 na Gerard Moreno wa Villarreal ametoa pasi moja ya bao na amecheza mechi 13.

Luis Suarez wa Atletico Madrid ametupia mabao 7 akiwa amecheza mechi 10 huku Messi wa Barcelona akiwa ametupia mabao 7 na pasi moja ya bao kwenye mechi 14.

Benzema ambaye amekuwa haimbwi sana licha ya jitihada zake ndani ya uwanja amesema:"Nitazidi kupambana daima, nina amini kwamba mafanikio hayawezi kuja ikiwa nitashindwa kuongeza juhudi" .

3 COMMENTS:

  1. Hivi hii blog haina mhariri ama? Habari inamuhusu Karim Benzema lakini picha ni ya Gareth Bale hilo nalo ni la kuelekezwa?Na hii si mara ya kwanza suala hili kujirudia.Mnajishushia hadhi

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hawaii ndio waliikuwa wanapiga chabo chuoni,
      Field walienda kucheza tu, na haya ndio matokeo yake.

      Delete
  2. Hata mim siwaelewagi SALEH JEMBE na jopo lake sijui wanakunywaga kwanza ndo wanaenda kuchapisha stor zao,maana kama ni habar zingekuw zinapita kwa mharir zinachujwa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic