December 15, 2020

 


DEOGRATIUS Munish maarufu kama Dida sasa atakuwa ni mali ya Ihefu FC inayoshiriki Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2020/21.


Kipa huyo ambaye amewahi kuitumikia Klabu ya Simba msimu wa 2018/19 na kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara aliwahi pia kuwa kipa namba moja ndani ya Klabu ya Yanga.


Baada ya kuachwa na Simba alitumika ndani ya Klabu ya Lipuli FC ambayo kwa sasa imeshuka Ligi Kuu Bara na inapambana kurejea ndani ya ligi ikiwa inashiriki Ligi Daraja la Kwanza.


Habari zinaeleza kuwa Dida anaibuka ndani ya Ihefu FC kuongeza nguvu kwenye lango kutokana na timu hiyo kuwa kwenye mwendo wa kusuasua.


Ikiwa imecheza jumla ya mechi 15 imefungwa jumla ya mabao 18 na imefunga mabao 6.


Kocha Mkuu wa Ihefu FC, Zuber Katwila amesema kuwa kwenye dirisha dogo wanahitaji kusajili wachezaji wenye uzoefu ili kuongeza nguvu ndani ya kikosi hicho.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic