December 15, 2020

 


INGIZO jipya ndani ya kikosi cha Yanga kwenye dirsha dogo ambalo limefunguliwa leo Desemba 15, Saido Ntibanzokiza ameanza mchezo wake wa kwanza kwa kufunga mabao mawili ndani ya Uwanja wa Liti.

Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Cedric Kaze imecheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Singida United, Uwanja wa Liti na kushinda mabao 3-0.

Mabao ya Yanga yalifungwa na Saido dakika ya 22 na dakika ya 66 kwa mkwaju wa penalti na lile la tatu lilifungwa na Deus Kaseke dakika ya 81.

Baada ya mchezo wa leo ambao umeshuhudiwa na mashabiki wengi,nyota huyo amesema kuwa bado anaamini kwamba kuna nafasi ya kufanya vizuri kwenye mechi zijazo ndani ya uwanja.

"Kazi inaanza na kuna nafasi ya kufanya vizuri kwenye mechi zetu zijazo hasa ukizingatia kwamba kila mchezaji anaonyesha ushirikiano ndani ya uwanja.

"Tumeanza vizuri hatuna mashaka katika hili na unapoizungumzia Yanga ni timu kubwa hivyo nasi tunaamini kwamba tutafanya makubwa," amesema.

8 COMMENTS:

  1. Subiri wazee wa misumari waingie kazini

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ndio ulichojaliwa kujua tu darasa la nne wewe,Mambo ya kijijini kwenu unaleta huku "poor mind"

      Delete
    2. Makalio ya mama'ko nguchiro we!!
      Yaani unazani mimi ni mkonongo mwenzio toka porini kama wewe.Huwezi linganisha elimu yangu na darasa la saba lako tena la kijijini.

      Delete
  2. Sawa wa kijani na njano
    Kwa kumsifia ligikuu bado ameokota hayo magoli mawili basi hatulali.

    ReplyDelete
  3. Elimu huonekana kwa matendo Tena yanayofaa kwa jamii na mhusika mwenyewe kwa hapa msitaje Elimu.Wote mmmmmmm

    ReplyDelete
  4. Anaonekana Ni mchezaji nzuri lkn kwa kiwango Cha kawaida akija Simba Hana namba huyo ukiangalia hata mchezo ulivyokuwa Ni wa kawaida yanga walichagua team dhaifu ipo kundi b halafu nafasi ya 9 itakupa kipimo ghani ingawa baadhi ya wachezaji wake kama viungo wapo vzr Ila beki na forward Ni shida nimeongea kiuchambuzi sio kishabiki

    ReplyDelete
    Replies
    1. Umeongea kishabiki mno na sio kiuchambuzi na ndo maana umesema angeenda Simba angekosa namba..Lakini kwa taarifa yako, viongozi wa Simba walimfuata Burundi kujaribu kumrubuni ili arudishe pesa ya Yanga na asajiliwe Simba. Muwe mnatunza kumbukumbu vizuri wajameni

      Delete
  5. Mbona Chama anang'aa mechi mbovu hatusemi

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic