December 24, 2020


 KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, raia wa Ubegiji amesema kuwa hajafurahishwa na matokeo aliyoyapata kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya FC Platinum ya Zimbabwe.


Mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Taifa wa Zimbabwe ulikamilika kwa dakika 90 kwa mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Bara kushindwa kuweka mzani sawa.


Licha ya kufungwa dakika ya 17 na Perfect Likwende kutokana na mabeki kuzidiwa ujanja na nyota huyo wa FC Platinum ngoma ilikamilika kwa Simba kupoteza mchezo wa kwanza.


Ina kazi yakufanya kwenye mchezo wa marudio unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa Januari 5 kwa kutakiwa kuwa na chaguo moja la kushinda mabao zaidi ya mawili ikikwama hapo itakuwa imetolewa jumlajumla kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.


Sven amesema kuwa wachezaji wake hawakuwa makini jambo ambalo litawafanya wawe makini kwenye mchezo wa marudio


"Tunapaswa kuwa makini zaidi kwenye mchezo wa marudio kwa sababu tulistahili kushinda kwenye mchezo wetu ambao tulitawala kwa asilimia kubwa.

"Sijafurahishwa na matokeo ambayo tumeyapata ugenini hivyo tuna kazi ya kufanya mchezo wetu wa nyumbani," .


Mchezo wa jana Simba ilikosa huduma ya nyota wake John Bocco ambaye anasumbuliwa na majeraha huku Aishi Manula ambaye taarifa ya awali ilieleza kuwa hayupo fiti aliweza kukaa langoni.

9 COMMENTS:

  1. Kiukwel simba jana ilicheza chini ya kiwango sana hata mbinu za kocha wakati mwingine sio anatakiwa kuwa flexible kutokana na aina ya timu anayocheza nayo. Kwenye beki bado kuna tatizo na litaendelea kutugharimu kama club haitafanya usajili katika eneo la beki la sivyo bac kocha abadilishe mawazo yake namuona Ame akiokoa jahazi kama ataaminiwa na kocha. Wazee akina paschal na Onyango makosa kibao hakika jana wawa alistahili bakora za kutosha kutokana na makosa yake ya kujirudia rudia.

    ReplyDelete
  2. Hayo ni mawazo yako lakini kwa maana ya kucheza ugenini Simba hajacheza vibaya sana ila kosa moja la kuchelewa kukaba katika maeneo ndio limeigharimu simba lakini kwa muda mwingi simba ali control temper ya mchezo na alitengeneza nafasi nyingi za kufunga kuliko Platinum kwa hiyo ishu ya kusema simba imecheza vibaya kama vile simba inacheza nyumbani hiyo sio sawa na sasa hivi tushajua kuna kampeni chafu za media nyingi za kibongo kuidhoofisha simba kifikra na nafikiri simba watakuwa wameshajua lakini Simb hapa Dar es Salaam tukijipanga vizuri Platinum anafungwa si chini ya goli tatu.

    ReplyDelete
  3. Timu inacheza hovyo kabisa beki wote wazee wamechoka ukweli ndio huwo

    ReplyDelete
  4. Simba hawakucheza vibaya ila hawakutumia nafasi walizotengeneza. Mugalu aanze mechi ya marudiano...kama wanataka ushindi...wazimbabwe wana nidhamu kubwa ya kujilinda lakini wanafungika

    ReplyDelete
  5. In short tusidanganyanye, Simba sc haina beki kiujumla, Wawa, onyango wale sio mabeki wa kuzuia straiker mzoefu, angalia makosa ya Jana au mechi za ndani wanakuwa wazito Sana,
    Kingine hatuna wafungaji mtu Kama KAGERE, mugalu hao huwezi jiaminisha eti una mastraiker wakukupa MATOKEO, pia Kuna mtu Kama mzamiru huyu anatakiwa aondoke dirisha hili la usajili.
    Coach nae Hana mipango mkakati pale anapogungua mfumo alioupanga umefili, CHAMA Jana kumuanzinza Kama mfungaji lakini MATOKEO yake hakuna mpira aliotengenezewa mpaka akaamua kuanza kutembea uwanja mzima.
    CHANGAMOTO.
    1:SIMBA AFANYE USAJILI WA WAFUNGAJI WAWILI WA KIMATAIFA TENA HATARI ZAIDI YA WALIOPO
    2: wafanye usajili wa mabeki wawili imara zaidi wenye uwezo wa kuzuia na wawe wepesi
    HAPO TUNAWEZA TUKAFANYA VIZURI ZAIDI NA TIMU YETU YA SIMBA SC
    ikishindikana vpl msimu huu ndoto.
    FA ndoto na tusiwaze kuwatoa platinum

    ReplyDelete
  6. Kati ya wachezaji ambao Simba inatakiwa ijivunie ni mzawa Mzamiru sema tu mashabiki walio wengi wa Simba hawampendi, Ila kiufanisi Mzamiru anafanya kazi kubwa Sana na kwa ligi yetu namba anayocheza Mzamiru kwa wazawa hapatikan kilabu ingne.
    Leo unasema Mzamiru aondolewe nakuhakikishia utayakumbka haya nisemayo.
    Mzimiru ni injini kubwa.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwa ufanisi na ustawi wa Simba anatakiwa kuondoka, sawa Ni punda au mbogo ila mchezaji anayeongoza kuchomesha ndio yeye. Mfano mzur angalia Jana alipoingia kafanya mangapi ya ajabu

      Delete
    2. Ili goli litokee lazima kuwe na nakosa mkuu, hayo ni maoni yangu.
      Pia sisi hatuna taaluma ya mpira na mwalimu ndiye awezae kumrecommend abaki au aondoke.

      Delete
  7. Injini Ni j mkude, manula, shabalala, kapombe , CHAMA, Luis wakikosekana Simba hata ikicheza na singida utd haitoboi

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic