December 13, 2020


 BAADA ya kuelezwa kuwa kiungo mshambuliaji Mtanzania Shiza Kichuya amefungiwa kutocheza soka kwa muda wa miezi sita na Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), baba mzazi wa kiungo huyo, Ramadhan Kichuya ameitupia lawama Simba kwa kushindwa kukamilisha taratibu za uhamisho wa mchezaji huyo.

 

Kichuya alishitakiwa na klabu yake ya zamani ya Pharco ya Misri iliyomsajili mwaka 2019, kabla ya Januari mwaka huu kuibukia Simba na sasa anaichezea Namungo FC ya Lindi.

 

Wakati Kichuya akikutana na kifungo hicho Simba wao wamepigwa faini ya Dola 130,000 sawa na Sh 300m.


Baba Kichuya amesema:-“Awali Simba walimwambia kuwa aje Tanzania wao watamaliza taratibu zote lakini imekuwa tofauti.

 

“Makosa ya klabu ndiyo yanayosababisha matatizo kama hayo, ukichukulia mfano wale viongozi wa Simba walishamchoka kwa sababu walisema kiwango chake kilishuka mpaka kufikia muda wakampeleka kwa mkopo Namungo.

 

"Mimi naona hawatendi haki, wamesahau vile walikuwa wanamtegemea zamani.


 “Ila namuombea Mungu miezi hiyo iishe na arudi kwenye soka kwani ana kipaji na siyo cha kulazimisha,” alisema baba Kichuya.

 

Aidha, Kocha Mkuu wa Namungo FC, Hemed Morocco naye alisema kukosekana kwa mchezaji huyo ni pigo kwa timu hiyo ambayo itashiriki michuano ya kimataifa.


Chanzo Championi

12 COMMENTS:

  1. Uandishi kiazi kabisa haujui hata maana ya kubalance story, yaani unaandika habari kwa kusikiliza maelezo ya mtu mmoja hujamhoji Kichuya wala Simba halafu kesho unaleta story nyingine tofauti.
    Hiyo baba yake Kichuya si ameibuka baada ya mtoto wake kupata umaarufu kwani hamjui kuwa Kichuya alilelewa na nani na kwanini.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwani simba ndio imemlea kichuya?.wewe nani hadi umbishie baba mzazi?

      Delete
  2. Kwani baba mzazi akisema ndio final? Yeye hawezi kupotosha? Muhimu mwandishi angebalance story sio kutuletea habari ya upande mmoja. Angemwuuliza kichuya aluondokaje huko misri na kisha uongozi wa simba

    ReplyDelete
    Replies
    1. Maupotolo na mwandishi wao majinga yanadandia vitu kama vinawahusu

      Delete
  3. Mnajulikana hata kwa kugeza sahihi kumbuka Athumani Iddi

    ReplyDelete
  4. Kama yanga walivyokhushi sahih y Morison.

    ReplyDelete
    Replies
    1. kama kitu hujui ni bora kukaa kimya hakuna atakaejua kuwa wewe ni mbumbumbu kuliko kujifanya mjuaji halafu ukaonekana boya........kuna ushahidi gani ulishawahi kutolewa kuonyesha kuwa yanga waliwahi kugushi saini ya morrison?!!!!......hata kwenye ile kesi ya msingi iliyokwenda tff morrison mwenyewe alikiri mbele ya viongozi wa tff kuwa kweli sahihi ni yake.

      Delete
  5. Mwandishi hebu tueleze tff walimruhusu vip kichuya kucheza na kama alipata ITC nani aliyeotoa.huyu mchezaji alichelewa kuanza kucheza kwa ajili ya ITC baadae akaruhusiwa na baadhi ya vyombo vya habari viliripoti kuwasili kwa kibali hicho

    ReplyDelete
    Replies
    1. Asiyejua kuwa Tff inawabeba simba nani??!!!!,wameshaboronga mara nyingi,kama ambavyo walimwondoa morrisson kucheza yanga kwa madai kuwa usajili wake una mapungufu baadae wakaruhusu usajili wake simba kwa mapungufu kama yaleyale..... mapungufu yaleyale.......matokeo yake ndo hayo aibu inawakuta

      Delete
  6. Kichuya alikujaje simba bila uhamisho kukamilika?yy hajui sheria?alichezaje Simba na Namungo bila kibali cha uhamisho?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic