NDANI ya dakika 270,kipa namba moja ndani ya kikosi cha Mtibwa mzawa Aboutwaleeb Hamidu Mshery ameweza kukusanya clean sheet(cheza bila kufungwa) mara tatu mfululizo na kutimiza wajibu wake kwa kuipa pointi saba kati ya tisa.
Nyota huyo amekuwa imara ndani ya uwanja jambo ambalo linamfanya awe chaguo namba moja la kocha msaidizi, Vincent Barnaba ambaye anakiongoza kikosi hicho kwa sasa baada ya Zuber Katwila kubwaga manyanga na kuibukia Ihefu.
Ilikuwa Novemba 28, Mtibwa Sugar 0-0 Mbeya City mchezo wa pili ilikuwa ni Desemba 6,Mtibwa Sugar 1-0 Mwadui FC.Bao la Mtibwa Sugar lilifungwa na Riphat Khamis kwa shuti kali.
Kete yake ya tatu kukaa langoni na kuipa pointi tatu ilikuwa ni Desemba 11, Mtibwa Sugar 1-0 KMC bao la Mtibwa lilifungwa na Salum Kihimbwa kwa kichwa.
Mechi zote hizo ambazo mzawa huyo alikaa langoni zilichezwa Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.
Mtibwa Sugar Kwenye msimamo ipo nafasi ya 10 ikiwa na pointi 19 baada ya kucheza mechi 15.
Huu ni upimbi Manula ana clean sheet ngapi nitajie mechi ya.mwisho hakufungwa mfukulizo
ReplyDelete