December 25, 2020


 MAHAKAMA ya Usuluhishi ya Masuala ya Soka ya Kimataifa (CAS) kumtumia barua ya kumsimamisha kiungo mshambuliaji wa Simba, Mghana, Bernard Morrison kucheza soka hadi pale kesi yake itakaposikilizwa upya na hukumu kutolewa.

 

Hiyo ni baada ya Yanga kupeleka mashitaka yao CAS ikiomba sakata hilo kusikilizwa upya baada ya Kamati ya Sheria na Hadhi ya Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kumuamuru Morrison kuwa mchezaji huru na yeye kuamua kuibukia ndani ya Simba.

 

Kamati hiyo iliamuru Mghana huyo kuichezea Simba baada ya kubaini mkataba wake wa awali na Yanga kuonekana una mapungufu, maamuzi hayo yaliwafanya viongozi wa Yanga kukimbilia CAS kwenda kukata rufaa.


Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Spoti Xtra, kutoka ndani ya Simba, CAS imemtumia barua kiungo huyo ikimtaka kutoendelea kuitumikia timu hiyo katika mashindano yoyote ikiwemo Ligi Kuu Bara na Ligi ya Mabingwa Afrika.

 

Mtoa taarifa huyo alisema zaidi ya wiki moja na nusu sasa zimepita tangu kiungo huyo mwenye mbwembwe za kuupanda mpira kupokea barua hiyo ya kumzuia kuichezea Simba hadi pale kesi hiyo itakaposikilizwa na hukumu kutolewa na CAS.

 

Aliongeza kuwa, hiyo ndiyo sababu ya Simba kumuacha kiungo huyo kwenye safari ya Mbeya wakati Simba ilipokwenda kucheza mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Mbeya City, pamoja na Zimbabwe walipokwenda kucheza dhidi ya FC Platinum katika Ligi ya Mabingwa Afrika, huku pia akiukosa mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya KMC.

 

"Ukweli wa Morrison kuachwa kwenye msafara wetu uliokwenda kucheza dhidi ya Mbeya City mkoani Mbeya pamoja na huu wa Zimbabwe ni baada ya kupokea barua kutoka CAS.

 

"CAS walimtumia shauri la kusikilizwa kesi yake upya baada ya Yanga kumkatia rufaa wakiomba kusikilizwa upya kesi hiyo ambayo imekaa vibaya baada ya mahakama hiyo kumsimamisha kuitumikia Simba hadi pale itakaposikilizwa kesi hiyo na hukumu kutolewa.

 

"Hiyo ndiyo sababu kubwa ya Morrison kutokuwa sehemu ya mechi zetu kwa sasa, hakuna kingine,” alisema mtoa taarifa huyo.Hivi karibuni, Mwenyekiti wa Yanga, Mshindo Msolla, alisema: “Suala la Morrison tumelifikisha CAS baada ya TFF kumuamuru mchezaji huyo kuwa mali ya Simba, sisi tumeenda huko lengo ni kupata haki ambayo ninaamini tutapata," .

 

Morrison ambaye aliitumikia Yanga kwa takribani miezi sita, msimu huu alijiunga na Simba ambapo usajili wake huo ulileta mvutano mkubwa kiasi cha kufikishana TFF ambapo shirikisho hilo lilitoa majibu ya kwamba mchezaji huyo yupo huru kujiunga na timu yoyote baada ya kubaini mapungufu kwenye mkataba wake na Yanga.

9 COMMENTS:

  1. Nyie waandishi njaa mnalipwa pesa na yanga muandike ujinga.acheni kuwa mashonga.mamae

    ReplyDelete
    Replies
    1. Machen mambo haya, tafuteni kuzungumzia mambo msiyoyajua.

      Delete
  2. Mbona humtaji huyo kiongozi wa simba aliyekuambia? Unajitahidi sana kutumika labda njaa na mahaba binafsi vinakusumbua

    ReplyDelete
  3. Hizo taarifa ya barua ya Morrison ni kama ile ya kichuya kusimmishwa Namungo na simba kulipa fine.Wote senzo huyo ajue tu hii ni Tanzania na anatumika vibaya.

    ReplyDelete
  4. Leo muandishi katuingiza chaka kadanganya ktk dunia ambayo kwasasa ipo kiganjan hao yanga hat kulipia garama za uendeshaji wa hiyo kesi bado izo taarifa sio kweli pili FIFA hawawez kumzuia mchezaji kucheza mpira km kesi haijasikilizwa na wakat wote wa usikilizwaji labda mwandishi nae ana Cas yake apa bongo.ila tushingae sana mkesha wa sikukuu nao vyombo vinapigwa mno nahic sio yeye ni pombe za free izo

    ReplyDelete
    Replies
    1. Acha upoyoyo, Pakiwa na kesi kuhusu mtu, yy anakuwa nje ya mfumo, ndio maana mtumish akikutwa na kesi, anasimamishwa kaz hadi kesi isikilizwe, waikato huo wote anakosa sifa ya kuwa mtumishi.
      Sasa wewe unaongea ujinga,

      Delete
    2. Wewe ni mwelewa...big up

      Delete
  5. Mimi nasema senzo anatumika vibaya. Asubiri kipigo kinamnyemelea atakimbia nchi huyo

    ReplyDelete
  6. Mbona kichuya anaendelea kucheza?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic