December 25, 2020


 MSHAMBULIAJI wa APR ya Rwanda Jacques Tuyisenge, ambaye amekuwa akitajwa kuibukia ndani ya Klabu ya Yanga amesema kuwa kwa sasa haruhusiwi kuzungumza na timu yoyote kwa kuwa ana mkataba na tmu aliyopo.

Tuyisenge mwenye uraia wa Rwanda, aliwahi kutamba katika kikosi cha Gor Mahia akiwa sambamba na nyota wa sasa wa Simba, Meddie Kagere, Francis Kahata na Joash Onyango.

 

Nyota huyo kuhusu ishu ya kuhitajika na Yanga amesema: “Kwa sasa mimi ni mchezaji wa APR, siruhusiwi kufanya mazungumzo yoyote yanayohusu masuala ya usajili kwani kila kitu kinachohusu usajili wangu kinasimamiwa na meneja wangu Eto Mupenz.”

 

 Meneja wa mchezaji huyo, amesema kuwa bado hajapokea ofa yoyote kutoka Yanga inayomuhusu mshambuliaji huyo ambaye bado ana mkataba na APR.

 

"Tuyisenge bado ana mkataba wa kuendelea kuitumikia APR na kuhusu kutakiwa na Yanga bado sijapokea ofa yao na ambacho kinaongelewa kwa sasa ni tetesi tu, mazungumzo kamili hakuna,” alisema meneja huyo.


Chanzo:Spoti Xtra

4 COMMENTS:

  1. Kila mchezaji atasajiliwa na yanga kwa mujibu wa waamdishi uchwara wa bongo wanaolipwa na hao jamaa

    ReplyDelete
  2. Duu kila mchezaji anaenda yanga

    ReplyDelete
  3. Ukiamin kila liandikwalo humu basi utakuwa na tatizo la kufikiri na kupambanua mambo makubwa na madogo

    ReplyDelete
  4. Haha sasa asipoandika ninyi mtasoma nn au ku comment nn, ndo ivo tena.....

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic