December 11, 2020


 BAADA ya kutua Simba, kiungo mpya wa timu hiyo, Taddeo Lwanga amepewa program maalum na kocha wake, Sven Vandenbroeck ili kuhakikisha anakuwa fiti zaidi.

 

Lwanga raia wa Uganda, amesajiliwa na Simba kwa mkataba wa miaka miwili baada ya mchezaji huyo kuwa huru ikiwa ni muda mchache tangu atoke kuvunja mkataba na timu yake ya Tanta FC inayoshiriki Ligi Kuu ya Misri.


Amepewa jezi namba nne iliyokuwa inavaliwa na kiungo mkabaji Gerson Fraga raia wa Brazil ambaye kwa sasa anatibu jeraha la goti.


Jumatatu ya wiki hii, Lwanga alianza mazoezi na kikosi cha Simba, ambapo katika mazoezi ya Jumanne yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Simba Mo Arena, Dar, alionekana akikimbia tu mwanzo mwisho bila ya kugusa mpira kama wenzake.

 

Katika mazoezi hayo yaliyofanyika kwa takribani saa 1:30 na kushuhudiwa na Spoti Xtra, wakati yeye akiwa na progamu yake maalum ya kukimbia pekee kwa muda huo, wachezaji wengine wa Simba waliendelea na program za ndani ya uwanja ikiwa pamoja na kuchezea mpira.

4 COMMENTS:

  1. Bora yasitokew ya Kichuya ambaye alisema kavunja mkataba hukohuko Misri na leo hii anatuchafua

    ReplyDelete
  2. Bora yasitokew ya Kichuya ambaye alisema kavunja mkataba hukohuko Misri na leo hii anatuchafua

    ReplyDelete
  3. Kichuya anaichafua Simba au Simba inajichafua yenyewe. Kwenye bodi ya Simba kuna watu weledi na wazoefu kama Magori, Kaduguda kwa kuwataja wachache ni kwa namna gani walifanya kosa la wazi kabisa hata "layman" wa mpira hawezi kulifanya la kumsajili Kichuya kama mchezaji huru bila kufuatilia kwanza kwenye klabu yake ya Pharco kujua kama ameshavunja mkataba au la? Simu zipo, mitandao ipo na hata wangeamua kwenda na ndege hapo Misri tiketi ya kwenda na kurudi na malazi isingefika hata TZS 2M na wangepata taarifa za uhakika kabisa kabla ya kumsajili Kichuya. Sasa kwa ujuaji wao inabidi walipe takribani TZS 300M. Hata sakata la Morison walilikuza bila sababu ya msingi kwa kuwa walijua wameshamaliza mazungumzo ya siri na Morisson walishindwa nini kumsubiria amalizane na Yanga halafu ndio wamsajili badala yake wakatangaza wamemsajili wakati kesi ya Yanga na Morison ilikuwa bado haijaamuliwa. Matokeo yake kesi ya dakika tano ikachukua zaidi ya siku tatu kwa sababu watoa maamuzi walipata taharuki hasa ikizingatiwa nao ni washabiki wa hizi timu kubwa mbili.

    ReplyDelete
  4. Kiarabu kilimchanganya Kichuya, alijua kavunja mkataba kumbe mkataba bado unaendelea, umh...

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic