December 26, 2020


 MSHAMBULIAJIwa Yanga, Mghana, Michael Sarpong, amefichua kuwa atatumia umbo lake la urefu kwa kuhakikisha anafanikiwa kufunga mabao katika mipira ya faulo itakayopigwa na kiungo mshambuliaji mpya wa timu hiyo, Said Ntibazonkiza ‘Saido’ raia wa Burundi.

 

Sarpong ametoa kauli hiyo ikiwa mpaka sasa amefunga mabao manne katika mechi alizocheza msimu huu tangu ajiunge na Yanga kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Rayon Sports ya Rwanda.

 

Sarpong amesema kuwa, kitendo cha kuwa na mchezaji wa aina ya Saido ni faida kwake kwa kuwa atahakikisha anatumia umbo lake vizuri kwa kufunga mabao ya kutosha ambayo yatatokana na kupigwa mipira ya faulo.

 

"Nadhani kwangu kitu kikubwa ni kuisaidia timu kwa kuona inapata matokeo na ndiyo jukumu la kila mchezaji ndani ya kikosi chetu kwa sababu tunahitaji mafanikio ya pamoja hivyo kupambana kwetu kunatokana na mchango wa kila mchezaji kama unavyoona kwa Saido.

 

“Yule ni mchezaji mzuri ambaye kwetu atatusaidia kutokana na uzoefu na ubora ambao anao lakini kwangu nataka kuona natumia vizuri ubora wake hasa katika mipira ya faulo kwa kuhakikisha nafunga mabao ambayo yataweza kutusaidia kufikia malengo kama wanavyofanya wachezaji wengine kwa kutumia umbo langu,” amesema Sarpong.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic