December 12, 2020

 


CEDRIC Kaze, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa ataingia uwanjani leo Desemba 12 kwa tahadhari kubwa wakati wakusaka pointi tatu mbele ya Mwadui FC kwa kuwa anatambua ni watibua rekodi wazuri.


Yanga ikiwa imecheza jumla ya mechi 14 haijapoteza mchezo inakutana na Mwadui FC ambayo imeshinda mechi tatu na kupoteza mechi 10 ikipata sare moja.


Kaze ameweka wazi kwamba licha ya kasi aliyonayo anawakumbuka Mwadui walitibua rekodi ya Simba kutofungwa msimu wa 2019/20.


"Mwadui ni timu nzuri licha ya kwamba haipati matokeo chanya, niliifuatilia msimu uliopita ilitibua rekodi ya Simba kutofungwa hivyo nimewaambia vijana wawe makini.


"Tunahitaji ushindi ili tuzidi kuwa imara ila hatupaswi kuwadharau wapinzani wetu kwa namna yoyote ile lazima tunawaheshimu," .


Yanga ipo nafasi ya kwanza ina pointi 34 inakutana na Mwadui FC yenye pointi 10 nafasi ya 17.


Mchezo wa leo utachezwa Uwanja wa Kambarage,  Shinyanga.

4 COMMENTS:

  1. Kwani wakati mwinyi zahera akiwa kocha yanga ilipoanzia ugenini ikiwa haijafungwa si walianza kufungwa na mwadui kwa goli la Jacob Massawe au bila kuitaja Simba huoni raha

    ReplyDelete
  2. Unaposema ni watibuaji wazuri unatakiwa utoe takwimu kuwa wamefanya hivyo mara ngapi na kwa timu zipi lakini unapotaja Simba pekee unaonesha kukosa umakini kwenye kaxi zako.... Halafu mbona waandishi wa humu hamjirekebishi kila siku mnakosolewa lakini hata hambadiliki

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic