December 29, 2020


 MASAU Bwire, Ofisa Habari wa Ruvu Shooting amesema kuwa kikosi chao kitaendelea kutoa soka la darasani ili kuleta ushindani ndani ya Ligi Kuu Bara.

Akizungumza na Saleh Jembe, Bwire amesema kuwa mwendo wao ndani ya Ligi Kuu Bara hautazima kwa kuwa wana wachezaji wazuri pamoja na mwalimu mwenye uzoefu.

Ndani ya Ligi Kuu Bara, Ruvu Shooting ipo nafasi ya tano ikiwa imekusanya pointi 26 baada ya kucheza mechi 16.

Bwire amesema:"Tupo imara na hatuna mashaka ya kile ambacho tunakifanya ndani ya ligi mpaka pale tutakapofikia malengo yetu.

"Vijana wetu wanacheza kwa kujituma na morali ni kubwa ndani na nje ya uwanja hivyo mashabiki waendelee kutupa sapoti.

"Tutaendelea kutoa mpira wa darasani na kuonyesha juhudi ndani ya uwanja. Mashabiki wasiache kutupa sapoti bila kuchoka," .

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic